MCHUNGAJI MSTAAFU AMOS NDAKI ASEMA: MUNGU NDIYE MSHAURI WA KWELI


Na Mapuli kitina Misalaba

Mchungaji mstaafu wa kanisa la AICT Kambarage, Amos Ndaki, amewahimiza Wakristo kuendelea kumtumainia Mungu kwa imani ya kweli na kufuata mafundisho ya Biblia katika kila hatua ya maisha yao.

Akihubiri leo Agosti 4,2024 katika ibada ya Jumapili kwenye Kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga, Mchungaji Ndaki amesema imani ya kweli katika Yesu Kristo huleta mafanikio na faraja katika maisha ya kila mtu.

Ameeleza kuwa katika maisha ya kila siku, watu hupata ushauri kutoka kwa watu tofauti, lakini amesisitiza umuhimu wa Wakristo na jamii kwa ujumla kupokea ushauri unaoleta mafanikio.

Mchungaji Ndaki amesisitiza kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mshauri wa kweli, na ni muhimu kwa kila mtu kuendelea kuzingatia maandiko yake katika Biblia kama sehemu ya mwongozo wa maisha.

 Kwa kufanya hivyo, itasaidia kuepuka mambo yasiyofaa katika jamii ambayo yanaweza kusababisha kifo, ikiwemo vitendo vya ukatili, wizi, utapeli, na uzinzi.

Katika mahubiri yake, amewataka waumini waendelee kuimarisha imani yao na kuwa na matumaini katika Mungu, kwani hiyo ndiyo njia ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao na jamii kwa ujumla.

TAZAMA MAHUBIRIMchungaji Jonas Mwita akiongoza ibada ya leo Jumapili Agosti 4,2024 katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.Mchungaji mstaafu Amos Ndaki akihubiri katika ibada ya Jumapili leo Agosti 4,2024 kwenye kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.Mchungaji mstaafu Amos Ndaki akihubiri katika ibada ya Jumapili leo Agosti 4,2024 kwenye kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.Waumini wakiwa katika ibada ya leo Jumapili Agosti 4,2024 kwenye kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.
Katibu wa kanisa la AICT Kambarage Bwana Magu Mabelele akisoma matangazo katika ibada ya leo Jumapili Agosti 4,2024.






 

Previous Post Next Post