Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo Agosti 14, 2024 ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na Kwimba mkoani Mwanza na kushudia watendaji hao wakiendelea na mafunzo.
Akizungumza na Waandishi hao Wasaidizi ngazi ya Kata, Mhe. Rwebangira aliwataka kuzingatia mafunzo hayo ili nao waende kuwafundisha wachini yao lakini kubwa ni kuhusu dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la uboreshaji uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.
Akiwa Wilayani Misungwi, Mhe. Magdalena alishuhudia washiriki wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri.
Viapo hivyo vilifanyika mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Esther Anorld Marick.
Maafisa waandikishaji wasaidizi Ngazi ya Kata kutoka Kata zote za mkoa wa Mwanza wameanza mafunzo leo ambapo Agosti 21 wanaanza uboreshaji wa Daftari hadi Agosti 27, 2024.