Na Mapuli Kitina Misalaba
Taasisi ya Wanawake na Samia Shinyanga imefanya
tukio la kupanda miti na kutoa msaada wa taulo na sabuni katika Kituo cha Afya
Kambarage, Shule ya Msingi Ibadakuli, na Shule ya (Shinyanga Girls) Wasichana
Butengwa, zote zikiwa katika Manispaa ya Shinyanga.
Katika Kituo cha Afya Kambarage, taasisi hiyo imetoa
msaada wa sabuni kwenye wodi ya wazazi, na katika Shule ya Msingi Ibadakuli na
Shule ya Wasichana Butengwa, wamegawa taulo kwa wanafunzi wa kike.
Aidha,
wamepanda miti katika maeneo hayo ili kuboresha mazingira na kuongeza
uhamasishaji juu ya umuhimu wa usafi wa mwili na mazingira.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Samia Mkoa wa
Shinyanga, Husna Mashaka Ally, amesema zaidi ya miti mia moja imepandwa na
taasisi hiyo.
Viongozi wengine
wa Taasisi ya Wanawake na Samia Shinyanga wamesisitiza umuhimu wa usafi wa
mwili na mazingira, hususan kwa wanafunzi, ili kujenga afya bora na mazingira
safi kwa wote.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage Dkt.
Ernest Magula pamoja na walimu wa shule zilizopokea msaada, wameishukuru na
kuipongeza taasisi hiyo kwa mchango wao mkubwa wa kupanda miti na kutoa msaada
kwa wanawake na wasichana.
Baadhi ya wanawake waliopokea msaada wa sabuni
katika Kituo cha Afya Kambarage na wanafunzi katika shule hizo nao wameishukuru
taasisi hiyo kwa msaada waliopewa.
Tukio hili linaonyesha jitihada za Taasisi ya
Wanawake na Samia Shinyanga katika kuboresha mazingira na afya za wakazi wa
Shinyanga, hususan wanawake na wasichana.