TUZIISH 4R ZA RAIS SAMIA


           
Ifahamike kuwa MH.DK  SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa awamu ya sita aliingia madarakani 2021 kwa mujibu wa wa katiba ya Jamhuri  ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977  ibara   ya 37 ibara ndogo ya 5 ambayo  inabainisha kuwa  ikitokea Rais aliyepo madarakani akiaga dunia  makamu wake huapishwa kuwa  Rais na amiri jeshi mkuu wa  majeshi yote ya ulinzi na usalama;
Pia hata utaratibu  wa CCM  Rais  akiapishwa pia utaratibu  hufanyika ili kumkabidhi nafasi ya uwenyekiti wa CCM Taifa hivyo Rais Samia mara tu baada ya kuapishwa  uliitishwa mkutano mkuu na akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM taifa.


Kimsingi  huu wakati  ulikuwa mgumu sana kwa taifa  letu  kuondokewa na Rais  aliyepo madarakani nchi na wana nchi tuligubikwa na majonzi na huzuni kubwa baada  ya kuodokewa na aliye kuwa  Rais  DK JOHN MAGUFULI  Tukirejea  hotuba ya kwanza Mh. Rais DK SAMIA  alisema na nukuu
“Leo nimelemewa na kidonda kikubwa moyoni mwangu na mzigo mzito mabegani mwangu”.


Hii ina akisi namna gani  sote kama taifa tulikuwa kwenye majonzi na huzuni kubwa isiyo na kifani  nahii sio kwa ngazi ya Taifa bali hata katika familia zetu ikitokea  kuondokewa na mpendwa  hujawa na huzuni na  majonzi ,hivyo tulipitia kipindi kigumu  na chenye majaribu makubwa sana na nijambo la kumshukuru Mungu tulivuka salama katika hali ya umoja na mshikamano wa taifa letu.

KAZI NA MAJUKUMU  YA KWANZA YA RAIS SAMIA

Kwa kuzingatia  mazingira ya dharura  ambayo  MH.Dk SAMIA MSULUHU HASSAN. Akiapishwa kuwa Rais na mkuu wa nchi  alikuwa na majuku ya awail  ya fuatayyo.

Kuwaondolea hofu wa Tanzania. Hili kimsingi lilikuwa jukumu kubwa la kwanza  kama mkuu wa nchi kwa kuwa  wananchi walikuwa na mawazo mseto na hili alifanya kwa  ufasaha mkubwa kweye somo la urai tunajifunza kuwa kazi ya Rais ni mfariji mkuu wa nchi.

 
Mfano .kupitia salamu aliyo iasisi kuwa “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wote itikieni kazi iendelee” .Hii salamu ya kifalsafa iliakisi na kuwaondolea hofu  wananchi  na ilitupatia  matumaini kuwa kila jambo linalo fanyika na serikali liko katika mifumo ya kitaasisi na sio mtuu, hivyo wa Tanzania wote tulipata   ahueni kuwa  nchi iko imara  na  huu ni uthibitisho kuwa CCM iko imara na mathubuti.


Kazi ieendelee imeonekana katika kuimarika kwa Muungano wetu kama ulivyoasisiwa mwaka 1964  Pia hata katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikendeelea  kushika kasi mfano reli ya kikasasa SGR  DSM hadi DODOMA imeanza kazi, mraadi mkubwa wa umeme wa nyerere ufiji (NHEP) unaendelea,pia uendelezwaji wa mji wa serikali Mtuma Dodoma unaendelea na hata Ikulu ya Chamwino pia imemalizika  kujengwa. Haya ni kwa uchache tu hivyo watanzania hatuna budi. kumuunga mkono Rais samia  pamoja na CCM kwa ujumla.

Kuwaunganisha wa Tanzania hapa ndipo tunapoona mantiki ya R4. Hasa ile dhana ya maridhiano. (reconciliation)  kwa kuzingatia kuwa nyenzo kuu ya  maendeleo ni umoja na mshikamano kama taifa tuwe kitu kimoja kulijenga, Amani ikitawala inahuisha ari ya kazi na uzalishaji wa kiuchumi katika taifa,hivyo dhana ya maridhiano na upatanisho imekuwa nguzo kubwa ya kudumisha upendo na uzalendo wa nchi na pia heshima ya binadamu, ikumbukwe kuwa katika medali za siasa hapo awali kulikuwepo na zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katika kunadi sera na falsafa ya vyama na vyombo vya habari kuhisi kuto tendewa haki ya kuandika habari kwa uhuru kama ilivyo sheria  mara tu baada ya kuapishwa aliweza ruhusu shughuLi hizo zote kufanyika  kwa mujibu wa  katiba na sheria za nchi hii ili ashiria kwamba Rais analenga kuwaunganisha waTanzania wawe kitu kimoja (mshikamano)  ili kuleta maeendeleo. pia aliwaachia waliokuwa magerezani wale wenye kesi zenye mnasaba na siasa na pia kuwaita viongozi wa vyama vya  siasa kufanya nao mazungumzo  ambayo hatimaye hii imepelekea taifa kuwa na utulivu mkubwaa hapa tuna kila sababu ya kumpongeza MH.RAIS  SAMIA SULUHU HASSAN.

Kuimarisha diplomasia ya kikanda na dunia kwa ujumla na hususani diplomasia ya kiuchumi kwa mujibu wa sera ya mambo ya  nje  (Tanzania foreign policy) ya nchi yetu iliyo nzishwa mnamo 2001 ikichukua taswira ya kuimarisha diplomasia ya uchumi hususani kuvutia wawekezaji na technolojia na utalii ikiwemo utalii wa mikutano na matibabu  katika hospital ya Taifa Muhimbili na Benjamini mkapa Dodoma.


Kwa hili tumeshuhudia  mwaka 2019/2021  dunia ikiwa kwenye changamoto ya  UVICO 19  janga hili lili ifanya dunia kuwa katika mtanziko mkubwa wa diplomaisia  kwa mataifa mengi kufunga mipaka na kusitisha safari za ndege  na hata wale amabo hawakuapata chanjo ya uviko kuto ruhusiwa kuingia baadhi ya mataifa  ila kwa kutambua umuhimu wa kufungua nnchi toka katika  huo mtanziko  kwa kuruhusu chanjo ya UVIKO 19 hili liliashiria dhamira ya serikali kuhakikisha nchi ina ungana na dunia katika wajibu wa kujilinda dhidi ya majanga  yenye mmnasaba wa magonjwa na sio kujitenga kama kisiwaa.na kwa hili  hatuna budi kumpongeza Rais samia kwa kuwa kiongozi mwenye kujari na kuthamini Afya za binadamu na wanachi wake kwa ujumla.


Kujali haki za binadamu na utu wa mtu.hiiime dhihirika pale alipo ruhusu ma binti wanapo tokea kushika ujauzito na kujifungua kIsha warejee kwenye mfumo rasmi wa masomo  hili ni jambo kubwa lililoonyesha dhamira ya kweli ya mkuu wa nchi kujari utu wa mtuu na heshima yake.hili lime fungua njia kwa mabinti kueendelea na elimu  yao vizuri  pia tumeona Ujenzi wa shule maalum kwa   masomo ya sayansi kwa wasichana mfano Manyara girls.

TUZIFAHAMU 4R ZA RAIS SAMIA NA TIJA YAKE KWA UMOJA WA KITAIFA

1.MARIDHIANO (RECONCILIATION) hii ni kwamba sisi wa Tanzania tuweze kuishi  na kudumisha tunu ya Amani,umoja na mshikamano kwa kuzingatia msingi ya maridhiano kwa jambo au mitazamo mseto inapotokea. Na hii si kwa taifa bali hata ngazi ya familia  tukijenga desturi ya maridhiano tuta kuwa na umoja na mshikamano na hatimaye upendo miongoni mwetu nahii itapunguza migogoro   ya ndoa hata taraka kupungua ,hivyo falsafa ya maridhiano isibaki tu katika medali za siasa na vyama vya siasa bali tuiishi kwa vitendo katika jamii zetu. mfano tumeshuhudia  CCM mkoani Mwanza wakichanga fedha kwa ajili ya kumsaidia  ndg Tundu Lissu aweze kutengeneza gari yake hii imedhihirisha  kuwa kukinzana kimtazamo katika siasa hakuna madhara ya kushindwa kusaidiana katika mambo ya kijamii hili ni jambo la kupongezwaa na limedhihirisha kuwa CCM Kama taasisis ina iishi dhana ya maridhiano Na hii ndio siasa safi aliyo tu husia Baba wa taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba ili taifa lolote lipate maendeleo linahitaji siasa safi na uongozi bora hivyo CCM  imedhihirisha ina ishi kwenye msingi ya siasa safi.

2.USTAHIMILIVI  ( RECILIANT) Huu ni msingi wa demokrasia  kuvumiliana pale una pokosolewa na hii inasaidia kujenga taifa la watu wenye umoja na mshikamano. Mfano hai tumeshuhudia kiongozi mkuu wa nchi kubaki katika hali ya utulivu  na hatimaye hutoa majawabu  yasiyo ksi jazba wala kinyongo kwa wanao mkosoa.hii ina tuu fundisha kuwa ustahimilivu nunguzo muhimu sana katika siasa na jamii kwa ujumla.

 
Mfano  2023 tum shuhudia ukosoaji mkubwa  kuhusu mkataba wa bandari na  DPW  kuhusu uwekezaji, hata  taasisis nyingine  zika diliki ku msimamo wa kupinga lakini Mh.Rais SAMIA. Alibaki  kuwa mtulivu kwa kuwa ana fahamu tija na mantiki ya uwekezaji huu wa kimkakati kwa taifa letu.hii ime ashiria kuwa Rais samia ana ishi katika falsafa ya ustahimilivu   na huu ni uthibitisho tosha unao onyesha  kuwa ni kiongozi anayefanya siasa safi.

Kwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi  amethibitisha kuwa ustahimilivu ni nyenzo nzuri ya kuongoza  na kuishi na jamii nasi pia tuiishi hio zana ya ustahimilivu.


Sasa hata  katika familia zetu tuwe wavumilivu pale tunapopata changamoto ya kukosolewa hata tuwe tayari kusamehe.hii kwa  ufupi tunaita political  tolerance.

3.MAGEUZI  AU MABADILIKO.-(REFORMS). Hii dhana ina tuhimiza tuwe watu wa mabadiliko na tuwe tayari  kwamabadiliko. Hata historia ina tuonyesha kuwa  mwaka 1991 kwenye tume ya nyarari ili kuja na maoni ya wananchi juu ya mfumo wa chama kimoja    maoni  ya wananchi 21% walitaka mfumo wa vyama vingi na 79% litaka mfumo wa chama kimoja ueendelee  nah ii imethibitisha namna ilivyo kuwa vigumu watu kupokea mageuzi ya mifumo ila kwa namna  Mh Rais Samia anavyo zingatia mageuzi ya mifumo tumeona  kuundwa kwa tume mfano tume ya haki jinai. Hii yote ni kuhakikisha mageuzi yana kuwa ya kimifumo  kwa mstabali wa taifa.


Nasi  watumishi hatuna budi katika maeeneo yetu kuwa na uthubutu wa kufanya mageuzi  kwal dhummuni la kuishi hi falsafa ya mageuzi.

4.KUJENGA UPYA.(RE BULD).Hii falsafa ina tuasa kujenga upya pale ambapo pana changamoto ili tuweze kwenda mbele kama taifa.mfano tumeona mabadiliko ya sharia ya uchaguzi. T toka kuwa tume ya Taifa ya uchaguzina kuwa Tume Huru ya uchaguzi. Hii ni matokeo chanya ya hii falsafa ya kujenga upya.

HITIMISHO


Kimsingi Taifa letu lime kirimiwa kuwa na viongozi wa zalendo  na wenye mitazamo ya kifalsafa kulingana na alama za nyakati. Kuanzia kuasisiswa kwa taifa letu 1964   mapaka sasa taifa limeendendelea kuwa imara na mathubuti kwa kuwa viongozi wote wa chama na serikali wamekuwa wa kitoa kipaumbele swala la  kusimamia tunu za taifa letu, ikiwemo kueenzi muungano Kulinda amani na umoja wa kitaifa. Hivyo Rais SAMIA  amaekuwa mfuasi mahiri wa falsafa ya saiasa safi na uongozi bora hivyo Wa Tanzania Tumuunge mkono kwa kila mmoja wete kutimiza wajibu pale anapo fanyia shughuri,kwa pamoja tuna jenga taifa letu.


MAKALA HII IMEANDKWA NA
JOHN FRANCIS HAULE….0756717987
MKUU WA SOKO KUU LA ARUSHA

Previous Post Next Post