Zaidi ya Vijana 1000 wajitokeza katika kongamano la tunaruka na Mama Samia 2025 wilayani rorya ambapo kongamano Hilo limeandaliwa mahususi kwaajili ya kujifunza Fursa mbalimbali za kimaendeleo ndani ya wilaya ya rorya
Akizungumza na vijana wa Rorya Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe Jafari Chege amewataka Vijana kuitumia siku hii ya kongamano la kujikwamua kiuchumi kujifunza na kujiweka tayari kwaajili ya uwekezaji mbali mbali ndani ya rorya.
Baadhi ya wawezeshaji kutoka sekta mbalimbali wametoa mafunzo Kwa Vijana Hawa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana wilayani rorya.