WAZAZI mbalimbali Jijini Mwanza wanefurahia huduma za malezi kwa watoto wadogo zinazotolewa na shule ya mafunzo ya awali na msingi ya Betheli.
Walisema kupitia huduma hizo shuleni zinawawezesha kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kwa kuwa na uhakika wa watoto wao kuwa katika mazingira mazuri ya malezi ya maadili mema na masomo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Finias Mapesa alisema wanawapokea watoto wa kuanzia umri wa miaka mitatu na hulelewa kwa kufunzwa maadili mema ya kitanzania ikiwa ni pamoja na ya kidini.
Alisema masomo ya lugha zote Kiswahili na Kingereza hufundishwa kwa watoto kuanzia elimu ya awali huku wakionesha uwezo mkubwa katika kuelewa lugha.
Mapesa aliwataka wazazi kuwapeleka watoto katika shule ya awali ili waanze masomo mapema kwani inawajengea misingi mizuri ya kitaaluma katika maisha yao.