WATATU WAKAMATWA SHINYANGA KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI LESENI ZA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth S. Magomi 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kwa kushirikiana na Maofisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kujihusisha na kughushi nyaraka mbalimbali, zikiwemo leseni za watoa huduma ndogo za fedha daraja la pili (Microfinance), ambazo hutolewa na Benki Kuu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo ,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth S. Magomi, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Isack Maswi, Silyvester Lugata, na Selanyika Athumani.

Watuhumiwa hawa wanadaiwa kujihusisha na utapeli wa kuuza leseni bandia kwa watoa huduma ndogo za fedha, jambo ambalo limeleta athari kubwa kwa wafanyabiashara wanaohitaji leseni halali kutoka Benki Kuu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Maofisa kutoka Bank Kuu ya Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawatu ambao ni Isack Maswi , Silyvester Lugata na Selanyika Athumani kwa tuhuma za kujihusisha na kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo leseni za watoa huduma ndogondogo za fedha daraja la pili, yaani leseni za Microfinance leseni ambao zinatolewa na Bank Kuu”, amesema SACP Magomi.

Jeshi la Polisi limeonya juu ya athari za leseni hizi bandia kwa uchumi wa watoa huduma ndogo za fedha, na limewahimiza wananchi kuhakikisha wanapata leseni zao kutoka vyanzo rasmi pekee ili kuepuka kudanganywa na matapeli.

Kamanda Magomi ametoa wito kwa wananchi wote na wafanyabiashara wa Microfinance kuhakikisha wanatembelea Benki Kuu au matawi yake ya karibu wanapohitaji leseni za watoa huduma ndogo za fedha.

Pia, amewasisitiza kufika moja kwa moja kwenye tawi lolote la Benki Kuu iwapo wanahitaji msaada kuhusu upatikanaji wa leseni zao.
TAZAMA VIDEO
Previous Post Next Post