WATU wawili wilayani Magu Mkoani Mwanza wamejinyonga hadi kufa kutokana na mauaji waliyotenda kwa wenzao katika kipindi cha Mwezi Julai Mwaka huu.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo mbalimbali vya habari Jijini Mwanza Kamanda wa JESHI la POLISI Mkoani Mwanza Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa tarehe 28 Mwezi huu Lukonya Kisumo (3) wa Kijiji Cha Sayaka wilayani Magu aliuawa Kwa kunyongwa na Baba yake Mzazi.
Kamanda Mtafungwa alimtaja Kisumo Emmanuel (38) wa Kijiji Cha Sayaka ambaye baba Mzazi wa Mtoto huyo anayetuhumiwa kumnyonga mwanae na yeye akajinyonga hadi kufa.
Tukio jingine ni katika Kijiji Cha Kisamba Wilayani Magu ambapo Christina Kisinza (40) aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na mumewe aitwaye Ferdinand Mabula (41) wakati wakiwa wamelala chumbani kwa sababu ya wivu wa mapenzi baada ya hapo na yeye alikutwa akiwa amening'inia kwenye mti akiwa amekufa.