NA Bora Mustafa,
Misalaba Media, Arusha .
Afisa Miradi Arif Nooraly kutoka Shirika la Action Aids amesema Shirika hilo linaendelea kutoa elimu kwa jamii na kutahadharisha juu ya shughuli za kibinadamu zinazochangia mabadiliko ya tabianchi ili kufikia malengo ya Taifa na mpango wa Kidunia.
"Katika jitihada zetu tunatumia Wanawake na Vijana, tunaamini wana nguvu kubwa ya ushawishi katika utunzaji wa mazingira, na kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kutoa elimu kwa watu wengi zaidi, juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na namna ya kukabiliana nayo" amefafanua Nooraly.
Prof Elias Mutinda Mtalaamu wa kilimo hai amesema wananchi washirikishwe katika kutunza mazingira ikwemo kupanda miti, kutumia nishati safi, na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.
"Ikumbukwe zamani hali ya hewa ilikuwa safi na salama kwa binadamu tofauti na sasa, jamii ione wajibu kuyatunza mazingira bila kushurutishwa ili tuweze kuifikia kesho njema na kufanya kizazi kijacho kiepuke madhara makubwa yatokanayo na hewa ukaa" amefafanua Mutinda.
Aidha amesema wananchi wa vijijini ndio wanaoathirika zaidi na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi, kukosa mavuno ya kutosha kwa sababu ya mvua haba, mafuriko, joto kali na majanga mengine.
Dainesi Mtei ambaye ni Mratibu wa Wizara ya Kilimo amesema Mpango wa European Union Deforestation umesaidia kwa sehemu kubwa katika utunzaji wa misitu na kupunguza hewa ukaa.
"Kilimo ni maisha, na ni uti wa mgongo wa mtanzania, na Serikali kwa kutambua mchango mkubwa wa Sekta hiyo imeongeza bajeti kutoka Bilioni 900 hadi Tilion 1.48, na mazao yanayozalishwa katika shamba lililokatwa miti hayapokelewi katika soko la Nchi za Ulaya" ameeleza Mtei.
Aidha Mtei ameeleza kwamba Wizara inafanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuotesha miti, kupunguza uchomaji mkaa na kutumia nishati safi pamoja na kupunguza matumizi ya gesi chafu viwandani.
Mkulima anayejishughulisha na Kilimo hai kutoka Chamwino Ikulu Dodoma amewakumbusha wakulima wenzake, kuwatumia Maafisa Ugani, kulima kilimo hai cha matunda na mbogamboga pamoja na kutumia mbegu zilizothibitishwa.
Prof Elias Mutinda Mtalaamu wa kilimo hai amesema wananchi washirikishwe katika kutunza mazingira ikwemo kupanda miti, kutumia nishati safi, na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.
"Ikumbukwe zamani hali ya hewa ilikuwa safi na salama kwa binadamu tofauti na sasa, jamii inatakiwa kuona ni wajibu kuyatunza mazingira bila kushurutishwa ili tuweze kuifikia kesho njema na kufanya kizazi kijacho kiepuke madhara makubwa yatokanayo na hewa ukaa" amefafanua Mutinda.
Aidha amesema wananchi wa vijijini ndio wanaoathirika zaidi na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi, kukosa mavuno ya kutosha kwa sababu ya mvua haba, mafuriko, joto kali na majanga mengine.
Dainesi Mtei ambaye ni Mratibu wa Wizara ya Kilimo amesema Mpango wa European Union Deforestation umesaidia kwa sehemu kubwa katika utunzaji wa misitu na kupunguza hewa ukaa.
"Kilimo ni maisha, ni uti wa mgongo wa mtanzania, na Serikali kwa kutambua mchango mkubwa wa Sekta hiyo imeongeza bajeti kutoka Bilioni 900 hadi Tilion 1.48, na mazao yanayozalishwa katika shamba lililokatwa miti hayapokelewi katika soko la Nchi za Ulaya" lakini pia wa sasa tunauza nje kwa asilimia kubwa kahawa na parachichi, na mpango huu unakataa kuuziwa mazao yaliyotoka shamba lililokatwa miti" ameeleza Mtei.
Aidha ameeleza kwamba Wizara inafanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kuvuna maji ya mvua ili yasaidie katika kipindi cha ukame, kupima udongo na kuwaelimisha wakulima kutumia mbegu bora zilizothibitishwa.
Mkulima anayejishughulisha na Kilimo hai kutoka Chamwino Ikulu Dodoma amewakumbusha wakulima kuwatumia Maafisa Ugani, kulima kilimo hai cha matunda na mbogamboga pamoja na kutumia mbegu zilizothibitishwa.
Lakini pia Rahma Kiriwe Mwanaharakati wa Mazingira amesema wanatoa elimu kwa wanajaamii namna ya kutunza mazingira na pia kufikisha ujumbe kwa kutumia mitandao ya kijamii na makongamano mbalimbali yanayohamasiaha kuhamasisha kutunza mazingira .
Mwisho.