Padri Nicolaus Ngowi wa shirika la Damu Azizi ya Yesu amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea alasiri ya leo mkoani Kilimanjaro.

Taarifa rasmi ya kifo chake imetolewa na Mkuu wa shirika Provisio ya Tanzania, Pd Vedasto Ngowi.


Wakati huo huo Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chediel Sendoro amefariki dunia usiku huu, Septemba 9, 2024 baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA