Ticker

6/recent/ticker-posts

AJALI YAUA TISA WILAYANI MBARALI, WANANCHI WALIA NA SERIKALI UBOVU WA BARABARA




NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Alfredy Baharia Mwidunda (50) dereva na mkazi wa Ubaruku wilayani Mbarali aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.896 DHK aina ya Yutong basi la abiria mali ya kampuni ya Shari line lililokuwa likitokea Sumbawanga kuelekea Ubaruku Wilaya ya Mbarali.


Akizungumzia ajali hiyo baada ya kuzulu eneo la tukio, kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Benjamin Kuzaga, amesema mnamo Septemba 03, 2024 majira ya saa moja usiku huko katika kijiji cha Itamboleo Kata na Tarafa ya Chimala Mbarali katika barabara kuu ya Mbeya Njombe, Gari iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Alfredy Baharia Mwidunda [50], mkazi wa ubaruku iliacha njia kisha kugonga gema, kuanguka hatua iliyosababisha vifo vya watu tisa [09] kati yao wanaume 06 kati yao watoto 02, wanawake 03.

Kamanda Kuzaga amesema katika ajali hiyo watu 18 wamejeruhiwa kati yao wanaume 05, wanawake 13 na watoto 02.

Kuhusu chanzo cha ajali anasema ni uzembe wa dereva wa basi hilo kushindwa kulimudu gari hilo kwenye kona kali na hadi kuacha barabara na kutumbukia korongoni kisha kugonga gema. Dereva wa Basi hilo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni Chimala akiwa chini ya ulinzi wa Polisi na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya misheni Chimala na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya na wengine katika Hospitali ya Misheni Chimala wilayani Mbarali.

Polisi inaendelea kutoa wito kwa madereva kuwa makini kwa kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA

Post a Comment

0 Comments