Mkuu wa wilaya ya Musoma Ndg. Juma Chikoka ametembelea kisiwa cha Rukuba kilichopo Halmashauri ya musoma Mkoani Mara baada ya tukio la kinyama lilitokea kwa mwanamke mmoja kupigwa na mumewe kwa Shoka na kujeruhiwa kisha mwanaume huyo kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza katika mkutano na wakazi wa maeneo ya Rukuba Mhe Chikoka amewaagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulika na kuhakikisha Mharifu huyo anapatikana iwe kwa kukamatwa au kujisalimisha.
Aidha matukio ya unyanyasaji yamekuwa ni mengi maeneo ya visiwani kwani ulinzi na usalama umekua mdogo katika maeneo hayo.
Kisiwa cha rukuba kinatajwa kuwa kisiwa ambacho wakazi wengi wa maeneo hayo hawaifuati sheria kutokana na baadhi ya watu kuwa watukutu na kujichukulia sheria mkononi pindi wanapopatwa na majanga.