Katibu wa Umoja wa Waganga Tanzania (UWAWATA) Lucas Mlipu ameitaka serikali na wadau wa maendeleo ya jamii kuwasaidia katika masuala mbalimbali Ili wakidhi mahitaji mbalimbali kwenye
kazi zao.
Alisema hayo katika kilele Cha maadhimisho ya Tiba asili kwa kuitaka jamii itofautishe baina ya Waganga wa Tiba asili na Matapeli wanaotumia mwamvuli wa Tiba asili,
Aidha ameomba Waganga wa Tiba asili washirikishwe kwenye vikao vya maamuzi na kuwa na Msemaji Bungeni.
Mlipu aliomba waganga wa Tiba asili, wanaorithi na kurithishwa uganga kwa Mjibu wa mwongozo wa Sheria na 23/2002 waruhusiwe kurithi baadhi ya nyara chakavu kama kiunganishi cha uasili huu unatambulika kisheria kwa sasa.
Hata hivyo alisema wanapashwa wapewe Elimu ya kuzitumia kwa kufuata maelekezo ya kisheria kutoka Mamlaka husika.
Aliongeza kusema serikali itenge Maeneo ya kupanda miti dawa kwa kila Halmashauri hapa nchini, kwa lengo la kuzalisha miti dawa kwa kwa ajili ya kuchakata dawa katika viwanda vyetu na kuwa na uzalishaji mkubwa wa dawa asili nchini:
UWAWATA inaamini kuwa Changamoto hizi zikitatuliwa Tiba asili itakuwa na muendelezo chanya kwa nchi yetu na Jamii kwa Ujumla ambao Watakuwa Wanaotumia dawa za asili hapa nchini.
Alisema Vyama vya Tiba asili, vimekuwa na Utendaji mugumu katika maeneo ya Halmashauri zote nchini hivyo kuwepo mazingira rafiki ya ufanyaji kazi Kwa waganga wa tiba asili ni mhimu.
Alishauri Vyama vya waganga vipewe ushirikiano wa kutoa Elimu kwa Wanachama wao kwa vikao vya Elimu ya ndani na mikutano ya hadhara kwa lengo la kuielimisha Jamii kutambua dalili na mbinu za matapeli.
Mlipu alisema majadiliano yanayohusu Tiba asili na Waganga wa Tiba asili yafanywe kabla ya Serikali kutoa Maamuzi.
Vilevile Katibu ameomba Serikali ipange Bajeti ya kwa kila Mwaka kuwezesha Zoezi la Upandaji miti dawa hapa nchini Ili waganga tiba asili watumie katika matibabu yao.
Kwa upande wa Matukio ya Matapeli wanaotumia mwamvuli wa Tiba asili
Katibu Mkuu UWAWATA Lukas Mlipu, amesikitishwa na amelaani vikali vitendo viovu vya kikatili vinavyoendelea hapa nchini, vikiwemo baadhi ya matapeli kutumia mwamvuli wa Tiba asili, kushiriki kufanya ushirikiana wa Kuwauwa watu.
Alisema pia matapeli hao baadhi yao kufanya mauaji kwa wateja wao , aidha kwa Tamaa za Fedha, na wengine kulawiti Watoto wao kwa Imani wanazoaminishwa na Matapeli hao eti watapata Mafanikio ya Mali au madaraka.
Katibu huyo amesema waganga ambao ni matapeli wamekuwa wakiwadanganya watu kwa kuhitaji mali zote za walengwa, viungo vya binadamu kama sharti la kupata utajiri hivyo watu wanapowaona watu wa Namna hiyo wawakatae.