ASKOFU SANGU KESHO KUPOKEA MICHANGO YA JEJIKASHI NA ILE YA KUANZISHWA KWA JIMBO JIPYA LA BARIADI

Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho Jumanne tarehe 01.10.2024, ataongoza Misa takatifu ya Kijimbo ya kilele cha uwasilishaji wa michango ya kulitegemeza Jimbo (JEJIKASHI) pamoja na ile ya maandalizi ya kuanzishwa kwa Jimbo Jipya la Bariadi.

Kwa mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Richard Makoye, Misa hiyo ambayo itafanyika katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga, itaanza saa 4:00 asubuhi.

Kupitia Misa hiyo, Parokia zote pamoja na taasisi za Jimbo, zitawasilisha mbele ya Askofu michango hiyo iliyokusanywa kwa kipindi cha mwaka huu 2024, ambayo itatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya Jimbo pamoja na maandalizi ya kuanzishwa kwa Jimbo jipya la Bariadi, ambalo litatokana na kumegwa kwa sehemu ya Jimbo la Shinyanga .
Previous Post Next Post