Na Mapuli Kitina Misalaba
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania
(AICT), Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota, amewakumbusha Wakristo kuendelea
kumtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yao ya kila siku ili kuepukana na maovu
ya dunia.
Akihubiri katika ibada ya Jumapili iliyofanyika leo,
Askofu Bugota amesisitiza umuhimu wa Wakristo kuishi kwa kumtumainia Mungu na
kuliombea taifa la Tanzania, ili kuondokana na vitendo vya ukatili kama vile
mauaji, watu kupotea, na kutekwa nyara, matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa
mara kwa mara katika mikoa mbalimbali nchini.
Aidha, Askofu Bugota amewahimiza watumishi wa Mungu,
wakiwemo wachungaji na wainjilisti, kuendelea kutoa mafundisho yanayojenga
jamii ili kuepusha kuenea kwa maovu ya kidunia.
Ameonya dhidi ya mambo ya kishirikina na kuwataka
waumini kuwa wavumilivu, wakimtegemea Mungu, huku wakiamini kuwa maombi yao
yatapata majibu.
Askofu Bugota amesema kubadilisha tabia na kuwa na
maadili mema kunahitaji maombi ya dhati kwa wale wanaohitaji kujitambua, huku akihimiza
umuhimu wa kuendelea kuombea mabadiliko chanya katika jamii.
Ibada hiyo imeambatana na nyimbo za sifa na kuomba kwa ajili ya amani na ustawi wa taifa.
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT), Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota, akihubiri katika ibada ya Jumapili leo Septemba 01,2024.
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT), Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota, akihubiri katika ibada ya Jumapili leo Septemba 01,2024.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Kambarage, Charles Lugembe akiongoza ibada ya Jumapili leo Septemba 01,2024.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Kambarage, Charles Lugembe akiongoza ibada ya Jumapili leo Septemba 01,2024.
Bwana Maligisa James Dotto akisoma matangazo ya kanisa kwenye ibada ya Jumapili leo Septemba 01,2024.
Bwana Maligisa James Dotto akisoma matangazo ya kanisa kwenye ibada ya Jumapili leo Septemba 01,2024
Ibada ya Jumapili ikiendelea katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga leo Septemba 01,2024.