Mwandishi wa habari Mkongwe nchini Michael Sikapundwa ambae amawahi kuandikia Magazeti mbali mbali makubwa nchini kutoka mkoa wa Morogoro amefariki Dunia kwa ajali ya gari.
Mwandishi huyo amefariki usiku wa kuamkia leo kwa ajali iliyotokea eneo la Tungi Morogoro na gari Hilo alikuwa akiendesha mwenyewe na hakuna na mtu mwingine.
Mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Tunaomba mwenye mawasiliano yeyote na familia yake aujulishe Uongozi wa Morogoro Press Club, Polisi Moro, ama waweza Wasiliana na mwandishi Idda Mushi 0754296927.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro zinaendelea ili kujua chanzo hasa Cha ajali hii na taarifa zaidi .
CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA