Ticker

6/recent/ticker-posts

DCEA KASKAZINI WATEKETEZA MIRUNGI

 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishna Jenerali tarehe 13.09.2024 imeteketeza kwa mujibu wa sheria vielelezo vya dawa za kulevya aina ya mirungi kilogramu 23.74 zilizokamatwa katika operesheni zilizotekelezwa hivi karibuni. Uteketezaji wa vielelezo hivyo ulifanyika katika Dampo la Murieti jijini Arusha. 


Zoezi hilo pia limeshuhudiwa na wawakilishi kutoka Mahakama ya Wilaya, ya Arusha, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, Ofisi ya Mkemia Mkuu zote kutoka Mkoani Arusha kulingana na matakwa ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. 








Post a Comment

0 Comments