EACS KITOVU CHA VIFAA VYA MGODINI, VIWANDANI

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kisasa kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS), Peter Andrew Kumalilwa akieleza namna wanavyozalisha vipuli vya mitambo (Steel Conveyor Rollers)
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS) Mhandisi  John Kubini (kulia) akionesha vipuli vilivyotengenezwa katika kiwanda cha EACS kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga

Na Kadama Malunde 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kisasa kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS), Peter Andrew Kumalilwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji hali iliyochangia kuaminika kwa bidhaa wanazozalisha kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na ubora unaokidhi viwango vya ushindani katika Soko la ndani na nje.

Kumalilwa ametoa Shukrani hizo leo Alhamisi Septemba 26,2024 wakati Maafisa kutoka Wizara ya Madini Kitengo cha Habari walipotembelea Kiwanda cha EACS kilichopo katika eneo la Mgodi wa zamani wa Buzwagi Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga ambalo limebadilishwa kuwa eneo maalumu la Uwekezaji Kiuchumi (Buzwagi Special Economic Zone) baada ya shughuli za uchimbaji madini zilizokuwa zikifanywa na Kampuni ya Barrick kufikia tamati.

“Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira chanya kwa ajili ya uwekezaji, bila yeye tusingeweza kuwa hapa, tulikuwa tunaona tu watu wengine wakifanya hivi vitu lakini katika awamu yake hivi vitu vimeanza kuonekana, Namshukuru sana pia Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ni msikivu, mpambanaji kwa kutuunga mkono kwa sababu kila wakati ukiwa na shida milango yake iko wazi, nawashukuru Tume ya Madini, Kamishna wa madini na tume nzima ya Wizara na viongozi mbalimbali”,amesema Kumalilwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha EACS Peter Andrew Kumalilwa 

Naomba niishukuru sana Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amekuwa Champion sana wa kuhakikisha hiki kiwanda kinasimama, yeye ndiyo aliyenisaidia kunikutanisha na mwekezaji kutoka Afrika Kusini ambaye nimeingia naye ubia kuanzisha kiwanda hiki na kuhakikisha kuwa Barrick wanaweza kutupa eneo hapa , nashukuru sana Serikali kwa kuweza kunibeba mgongoni. Nawashukuru sana Barrick na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan maana bila yeye kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ingekuwa ngumu sana kumshauri mwekezaji kutoka nje ya nchi yake kuja kuwekeza Tanzania”,ameongeza Kumalilwa.


Ameeleza kuwa, Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited EACS kinatengeneza Vipuli vya mitambo (Steel Conveyor Rollers, Plastic Conveyor rollers & Steel Frame) ambapo malighafi nyingi mfano za Steel na nondo zinatoka katika viwanda vilivyopo nchini Tanzania na kwamba vipuli hivyo wanavipeleka kwenye Migodi mbalimbali ikiwemo Barrick North Mara na Barrick Bulyanhulu na migodi iliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia.

Sisi East Africa Conveyor Supplies Limited tunatengeneza bidhaa zenye kiwango cha hali ya juu ndiyo maana tusambaza pia kwenye Migodi ya Barrick North Mara na Bulyanhulu ambao wanazingatia sana viwango vya ubora”,ameongeza Kumalilwa.
Sehemu ya vipuli vilivyotengenezwa katika kiwanda cha EACS

Kumalilwa amefafanua kuwa, kutokana na kwamba bidhaa wanazozalisha ni bora ,nchi mbalimbali zimevutiwa na bidhaa hizo na hivi karibuni wanaratajia kupanua soko lao hadi nchi za Afrika Magharibi.

Aidha ametoa rai kwa Taasisi za Kifedha ziwaangalie Watanzania ambao wamejikita kwenye usambazaji wa vipuri au wanaoanzisha viwanda vya kutengeneza vipuli kama EACS wawape mikopo ya riba nafuu ili waweze kuingia kwenye ushindani na kuungana na wawekezaji wa nje mfano kama EACS walivyoingia makubaliano ya kuweka fedha nusu na mwekezaji kutoka nje ya nchi.

Aidha amewaomba wawekezaji wa sekta ya madini na viwanda vya uzalishaji wa saruji nchini kutumia vipuli kutoka EACS vinavyozalishwa nchini ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.
Shughuli za utengenezaji Vipuli zikiendelea katika kiwanda cha EACS

Migodi mingi na viwanda vingi vinahitaji sana Steel, naomba Viwanda viwekeze kwenye uzalishaji wa steel bora ili tuweze kutengeneza hizi bidhaa zetu kwa sababu Steel inatumika kwenye vitu mfano kwenye migodi mitambo mingi imetengenezwa kwa steel. Natoa wito kwa Watanzania wachangamkie hii fursa ikizingatiwa kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhihirisha kwamba yeye anataka sana Wazawa waweze kutengeneza viwanda ili tupate ajira ya watu wetu”,amesema Kumalilwa.

Amesema Vipuli ni moyo wa kiwanda hivyo bidhaa wanazozalisha zinaweza kutumika kwenye migodi, viwanja vya ndege, viwanda mbalimbali vikiwemo vya saruji hivyo ametoa rai kwa Viwanda mbalimbali kama vya Dangote wapate bidhaa bora kutoka EACS lakini pia migodi mbalimbali kama Geita Gold Mine, Shanta Mining wafanye kazi na EACS kwa kutumia vipuli kutoka EACS.

“Nataka niwasisitize Watanzania kuwa Madini ni maisha, changamkieni hizi fursa, tusibake tu mijini, tuje huku kwenye migodi tuangalie fursa gani tunaweza kufanya hasa tukiweza kushirikiana na watu wa nje ya nchi au kama tunaweza kufanya sisi wenyewe kwa asilimia 100. Tunataka kuhakikisha viwanda vingi vinaongezeka ili kufanya usambazaji kwenye migodi na kuhakikisha hiyo shilingi Trilioni 3.1 kila mwaka inapita katika Watanzania ili kukuza uchumi”,amesema.

Naomba Watanzania wachangamkie fursa ya usambaji, tumeambiwa kila mwaka kuna shilingi Trilioni 3.1 inayopita katika mnyororo wa thamani, kama wazawa hawatakuja mbele fedha itaenda nje ya nchi. Naomba sana tuweze kushikana mikono na tuhakikishe tunafungua viwanda vingi na kusambaza ujuzi na kuwapa ajira watu wetu”,amesema Kumalilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wasambaji Vipuli vya migodini nchini (Tanzania Mining Industry Suppliers Association -TAMISA).

ALIPATA WAPI WAZO LA KUANZISHA KIWANDA CHA VIPULI?

Kumalilwa amesema alipata wazo la kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vipuli baada ya kuona kwenye Usambazaji wa vipuli ambazo nyingi zilikuwa zinaenda kwa Wageni zaidi ambapo vifaa vingi vilikuwa vinaletwa kutoka nje ya nchi.

“Mimi ni Local Partner wa Kampuni ya EACS. Nipo kwenye sekta ya madini tangu mwaka 1997, mwanzo nilikuwa kwenye Kampuni nyingine baadaye migodi mingi ikafunguliwa tukaanza kuona fursa kwenye Usambazaji wa vipuli ambazo nyingi zilikuwa zinaenda kwa Wageni zaidi, vifaa vingi vilikuwa vinaletwa kutoka nje.

Nikiwa kwenye moja ya mikutano nchini Afrika Kusini nilikutana na mmoja wa Wawekezaji aliyekuwa anafanya kazi na Migodi ya Barrick Afrika nzima, nikamwelezea kuhusu Local Content, kwa msaada pia wa Wizara ya Madini aliweza kuja Tanzania na kwa msaada wa Barrick waliweza kutupa hili eneo la Buzwagi ili tuweze kuanzisha hiki kiwanda, kiwanda chake cha World Wide Conveyor kilichokuwa Afrika Kusini lakini akafunga shughuli zake zote akaleta hapa Buzwagi tukafungua hii East Africa Conveyor Supplies Limited”,ameeleza Kumalilwa.
Meneja wa Kiwanda cha EACS Mhandisi John Kubini (kulia) akionesha vipuli vinavyotengenezwa katika kiwanda cha EACS

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS) Bw. John Kubini amesema Kiwanda cha EACS ambacho kimeanza shughuli za uzalishaji Mwezi Mei,2023 ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa nchini ambao umefungua fursa za kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini.

Wakiwa katika kiwanda cha EACS Maafisa kutoka Wizara ya Madini Kitengo cha Habari wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini Bi. Asteria Muhozya Alhamisi Septemba 26,2024 wamejionea namna kiwanda hicho kinavyofanya shughuli za uzalishaji vipuli ikiwa ni sehemu ya ziara yao kutembelea Viwanda vya Wawekezaji Wazawa wanaotengeneza vifaa vya migodini.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kisasa kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS), Peter Andrew Kumalilwa akieleza namna wanavyozalisha vipuli vya mitambo (Steel Conveyor Rollers) Septemba 26,2024 wakati Maafisa kutoka Wizara ya Madini Kitengo cha Habari walipofanya ziara kujionea namna kiwanda hicho kinavyofanya shughuli za uzalishaji vipuli ikiwa ni sehemu ya ziara yao kutembelea Viwanda vya Wawekezaji Wazawa wanaotengeneza vifaa vya migodini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kisasa kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS), Peter Andrew Kumalilwa akieleza namna wanavyozalisha vipuli vya mitambo (Steel Conveyor Rollers)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kisasa kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS), Peter Andrew Kumalilwa akieleza namna wanavyozalisha vipuli vya mitambo 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kisasa kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS), Peter Andrew Kumalilwa akiwakaribisha Maafisa kutoka Wizara ya Madini Kitengo cha Habari walipofanya ziara kujionea namna kiwanda hicho kinavyofanya shughuli za uzalishaji vipuli
Muonekano wa sehemu ya Kiwanda cha kinachozalisha Vipuli vya Mitambo cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS)
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS) Mhandisi John Kubini akionesha namna vipuli vinatengenezwa katika kiwanda hicho. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini Bi. Asteria Muhozya
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS) Mhandisi John Kubini (kushoto) akielezea kuhusu vipuli wanavyozalisha vipuli. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini Bi. Asteria Muhozya, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha EACS, Peter Andrew Kumalilwa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini Bi. Asteria Muhozya (kulia) akiangalia vipuli ambavyo vimetengenezwa katika kiwanda cha EACS vikiwa tayari kusafirishwa kwenda Congo na Zambia
Sehemu ya vipuli vilivyotengenezwa katika kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited (EACS) kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Maafisa kutoka Wizara ya Madini Kitengo cha Habari wakiangalia vipuli vilivyotengenezwa katika kiwanda cha EACS kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Meneja wa Kiwanda cha EACS Mhandisi John Kubini (katikati) akieleza namna wanavyotengeneza vipuli
Meneja wa Kiwanda cha EACS Mhandisi John Kubini (katikati) akieleza namna wanavyotengeneza vipuli 
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (kushoto) akielezea kuhusu utengenezaji wa vipuli
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (kulia) akionesha mitambo inayotumika kutengeneza vipuli katika kiwanda cha EACS
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (kulia) akionesha mitambo inayotumika kutengeneza vipuli katika kiwanda cha EACS
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (kushoto) akionesha mitambo inayotumika kutengeneza vipuli katika kiwanda cha EACS
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (kulia) akionesha moja ya vipuli katika kiwanda cha EACS
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (katikati) akielezea kuhusu utengenezaji wa vipuli katika kiwanda cha EACS
Meneja wa Kiwanda cha East Africa Conveyor Supplies Limited  Mhandisi John Kubini (kushoto) akielezea kuhusu utengenezaji wa vipuli katika kiwanda cha EACS
Shughuli za utengenezaji Vipuli zikiendelea katika kiwanda cha EACS
Shughuli za utengenezaji Vipuli zikiendelea katika kiwanda cha EACS
Shughuli za utengenezaji Vipuli zikiendelea katika kiwanda cha EACS
Shughuli za utengenezaji Vipuli zikiendelea katika kiwanda cha EACS
Malighafi ndani ya kiwanda cha EACS kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Muonekano sehemu ya kiwanda cha EACS kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Muonekano sehemu ya kiwanda cha EACS kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Muonekano sehemu ya kiwanda cha EACS kilichopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Previous Post Next Post