ENG. JUMBE AONGOZA MAHAFALI YA 53 SHULE YA MSINGI JOMU

 

Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa (kushoto) akikabidhiVifaa vya TEHAMA kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi, Pendo Himbi


Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa ametimiza ahadi yake ya kuchangia Vifaa vya TEHAMA ikiwemo Printers, Computers na Photocopy Mashine katika shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1964 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira shuleni.


Mhandisi James Jumbe maarufu Kaka Mkubwa katika shule hiyo, ametimiza ahadi yake leo Ijumaa Septemba 20,2024 wakati wa Mahafali ya 53 ya darasa ya saba ambapo alikuwa mgeni rasmi .

“Nimekuja kushiriki nanyi kwenye mahafali haya kama Mhitimu wa Shule hii (Alumni wa shule hii) kuchagiza chachu ya wahitimu kuona umuhimu wa kusaidia shule zao, naendelea kutoa wito kwa wengine kuiga mfano huu, kurudi kwa jamii waliyotoka.Hapa Jomu kulikuwa na changamoto ya vifaa vya TEHAMA ikiwemo Printers, Computers na Photocopy Mashine ambavyo mwaka jana (2023) nikiwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya darasa la saba niliahidi kuleta”,amesema Jumbe.

“Mliomba mashine moja tu lakini nimeleta mashine moja kubwa ya kisasa inayofanya shughuli nyingi, lakini nyingine ndogo kwa ajili ya ofisi ya Mkuu wa Shule, Kifaa cha Internet (WiFi), pia computer mbili kwa ajili ya mashine hizi ambapo vifaa vyote hivi vina thamani ya shilingi Milioni 6. Naamini vifaa hivi vitachangia kuongeza ufaulu katika shule hii”,ameongeza Jumbe.
Sehemu ya Vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Mhandisi James Jumbe Wiswa

Jumbe amefafanua kuwa anamuunga mkono Mhe. Rais Samia katika kuboresha mazingira ya shule kutokana na kwamba Rais Dkt. Samia anapenda nchi yake, ni mzalendo kweli kweli kwa sababu amewekeza rasilimali kubwa katika kuiwezesha elimu, amejenga madarasa ya kutosha katika shule nyingi nchini.

“Wakati namaliza shule ya msingi Jomu mwaka 2002 tulikuwa na majengo matatu lakini sasa tuna majengo mengi ya kutosha kwa hiyo sisi kama wadau lazima tuunge mkono mhe. Rais Samia katika harakati zake za kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata nafasi ya kusoma katika mazingira Rafiki ndiyo maana na mimi nasema siwezi kubaki nyuma kwa sababu Mhe. Rais sisi kama vijana wapiganaji anatutengenezea mazingira rafiki, tunafanya shughuli zetu, tunasafiri pasipo mkwamo wowote, tunafanya biashara, hatuna hofu yoyote ya kuweka pesa zetu Benki kwa hiyo na sisi tuna jukumu la kurudisha kwa jamii”,ameeleza Jumbe.

 Mhandisi James Jumbe Wiswa akisalimiana na Wahitimu wa elimu ya darasa la saba 2024

Kuhusu changamoto ya kukosekana kwa jiko la kupikia katika shule hiyo, Mhandisi Jumbe ameahidi kutengeneza jiko ili kumuunga mkono mhe. Rais Samia anayesisitiza matumizi ya nishati safi na salama akihimiza kuhusu matumizi ya Nishati mbadala ikiwemo matumizi ya Gesi.

Hali kadhalika Jumbe ameahidi kuleta meza rafiki katika shule hiyo huku akitoa zawadi zap apo hapo kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo kama motisha.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Jomu, Pendo Himbi ameendelea kuwashukuru wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Shule ya Msingi Jomu kuleta maendeleo akiwemo Mhandisi Jumbe, Kanisa la AICT Kambarage, TANESCO, SHUWASA na wadau wengine hali inayochangia kuleta mabadiliko makubwa shuleni ikiwemo kuinua taaluma.

Akisoma risala, mmoja wahitimu Happiness Mohamed amesema jumla ya wanafunzi 42 wamehitimu elimu ya msingi mwaka huu 2024 huku akizitaja baadhi ya changamoto zilizopo sasa kuwa ni utoro wa wanafunzi 3% unaosababishwa na kukosa uzio wa shule, ukosefu wa jiko la kupikia chakula cha wanafunzi na walimu na upungufu wa viti 8 na meza 6 za walimu kwenye madarasa mapya.
Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo Mjini Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa akivalishwa Skavu wakati wa mahafali ya 53 ya darasa la saba leo Ijumaa Septemba 20,2024 ambapo alikuwa mgeni rasmi
Maandamano ya Wahitimu wa elimu ya darasa la saba na wanafunzi wengine wa shule ya Msingi Jomu kuelekea ukumbini yakiendelea wakati wa mahafali ya 53 ya darasa la saba 2024

Maandamano ya Wahitimu wa elimu ya darasa la saba na wanafunzi wengine wa shule ya Msingi Jomu kuelekea ukumbini yakiendelea wakati wa mahafali ya 53 ya darasa la saba 2024
Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo Mjini Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa akisalimiana na Wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakati wa mahafali ya 53 ya darasa la saba 2024
Wahitimu wa elimu ya darasa la saba 2024 shule ya Msingi Jomu wakitoa burudani
Wahitimu wa elimu ya darasa la saba 2024 shule ya Msingi Jomu wakitoa burudani
Mgeni rasmi wakati wa Mahafali ya 53 shule ya Msingi Jomu ambaye ni mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo Mjini Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza kwenye mahafali hayo
Mgeni rasmi wakati wa Mahafali ya 53 shule ya Msingi Jomu ambaye ni mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo Mjini Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza kwenye mahafali hayo
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jomu, Pendo Himbi akizungumza wakati wa mahafali ya 53 ya darasa la saba leo Ijumaa Septemba 20,2024
Diwani wa kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga mHE. Hassan Mwendapole akizungumza wakati wa mahafali ya 53 ya darasa la saba leo Ijumaa Septemba 20,2024
Mhitimu Happiness Mohamed akisoma risala
Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa (kushoto) akikabidhi Vifaa vya TEHAMA kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi, Pendo Himbi

Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa (kushoto) akikabidhiVifaa vya TEHAMA kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi, Pendo Himbi
Sehemu ya Vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa
Wahitimu wa elimu ya darasa la saba na viongozi mbalimbali wakipiga picha na Mhandisi James Jumbe Wiswa
Wanafunzi wakitoa burudani kwenye mahafali ya darasa la saba 2024 katika shule ya Awali na Msingi Jomu
Wanafunzi wakitoa burudani kwenye mahafali ya darasa la saba 2024 katika shule ya Awali na Msingi Jomu
Mhandisi James Jumbe Wiswa na Wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakikata keki maalumu wakati wa Mahafali ya 53 ya Shule ya Awali na Msingi Jomu
Zoezi la kulishana keki maalumu wakati wa Mahafali ya 53 ya Shule ya Awali na Msingi Jomu likiendelea
Zoezi la kulishana keki maalumu wakati wa Mahafali ya 53 ya Shule ya Awali na Msingi Jomu likiendelea
Mhandisi James Jumbe Wiswa akigawa vyeti kwa wahitimu wa elimu ya darasa la saba shule ya Awali na Msingi Jomu
Mhandisi James Jumbe Wiswa akigawa vyeti kwa wahitimu wa elimu ya darasa la saba shule ya Awali na Msingi Jomu
Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole  akikabidhi zawadi ya cheti kwa Mmoja wa Waliokuwa Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Jomu iliyopo Mjini Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa 

Wazazi na wageni mbalimbali wakicheza muziki kwenye mahafali ya darasa la saba 2024 katika shule ya Awali na Msingi Jomu.
Wazazi na wageni mbalimbali wakiwa kwenye mahafali ya darasa la saba 2024 katika shule ya Awali na Msingi Jomu.

Previous Post Next Post