Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imekuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ndogo za Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Sekta ya Nishati Kusini mwa Afrika (RERA) vilivyoanza rasmi leo, tarehe 23 Septemba 2024 visiwani Zanzibar.
Mamlaka za Udhibiti kutoka Angola, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Eswatini, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania zimeshiriki vikao hivyo. Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imeshiriki kama mtazamaji kwa kuwa bado haijawa mwanachama wa umoja huo.
Vikao hivyo vitakavyofanyika kwa awamu mbili, kati ya tarehe 23-27 Septemba, na 8-11 Oktoba, 2024, vinajadili pamoja na mambo mengine, namna ya kuboresha shughuli za udhibiti wa nishati katika maeneo ya fedha, rasilimali watu, huduma kwa wateja, habari, mawasiliano na teknolojia ya habari. Masuala mengine ni kuhusu udhibiti kiufundi na kiuchumi ikijumuisha bei, tozo na viwango vya huduma kwenye sekta za umeme,