FURSA YA UDHAMINI: MAFUNZO YA UOKAJI NA UJASIRIAMALI KWA MWANZA NA KANDA YA ZIWA

 

Tuna furaha kubwa kuwakaribisha wadhamini kujitokeza kudhamini Mafunzo ya Uokaji na Ujasiriamali, yanayoandaliwa na MariaSuzy Bakery Experts (SME)kwa kushirikiana na SIDO. 

Mafunzo haya yamepangwa kufanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kuanzia tarehe 28/10/2024 hadi 01/11/2024.

Hii ni fursa adimu ya kutoa mchango wako katika kuinua sekta ya ujasiriamali kwa wanawake na vijana wa Mwanza na kanda ya ziwa. 

Mafunzo haya yanawapatia washiriki mbinu bora za uokaji pamoja na maarifa ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo.

Kwa nini udhamini?
1. Ongeza Uonekano: Kampuni yako itapata nafasi ya kuonekana na kushirikiana na wajasiriamali wapya wanaokuja juu katika sekta ya chakula na bidhaa za uokaji.
2. Kuleta Mabadiliko: Udhamini wako utachangia kukuza kipato cha wanawake na vijana, na kuwasaidia kujitegemea kiuchumi kupitia biashara ya uokaji.
3. Fursa za Matangazo: Majina ya wadhamini yatawekwa katika matangazo yote ya tukio, mabango, na vipindi vya radio vinavyohusiana na mafunzo haya.

Wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo ili kujua jinsi gani unaweza kushiriki:
- 0788 774 594
- 0715 224 264

Tunatarajia kushirikiana nanyi katika kufanya tukio hili kuwa la mafanikio kwa jamii yetu.
Previous Post Next Post