Ticker

6/recent/ticker-posts

HOSPITALI YA KAIRUKI YATOA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA YA KUONDOA UVIMBE BILA UPASUAJI KWA MADAKTARI BINGWA KUTOKA KENYA


Hospitali ya Kairuki imetembelewa na Jumuiya ya Madaktari wa Magonjwa ya wanawake kutoka nchini Kenya , Obstetrical and Gynaecological Society (KOGS) wakiongozwa na Rais wa jumuiya hiyo Dkt. Frederick Kireki pamoja na Dkt.Chetan Ramaiya Makamu wa Rais Mstaafu wa Chama Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina Mama Tanzania,The Association of Gynaecologists and Obstetricians of Tanzania (AGOTA)

Ziara hiyo imelenga kufanya utalii tiba ili kuboresha huduma za afya Afrika Mashariki na Duniani kwa ujumla.

Katika ziara hiyo ugeni huo umepata mafunzo juu ya huduma mpya naya kisasa itolewayo na Kairuki Hospital ya kuondoa uvimbe bila upasuaji kwa kutumia Mtambo wa High Intensity Focused Ultrasound (HIFU) Pamoja na huduma ya Uzazi Pandikizi inayoptolewa na Kairuki Hospital Green IVF.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Kairuki Dkt. Muganyizi Kairuki Amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili ikiwemo kufanya utafiti. "Ushirikiano wetu udumishwe lakini pia tuwe na Tafiti zetu wenyewe juu ya matibabu tofauti tofauti katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki."

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya hiyo ya Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya wanawake nchini Kenya Dkt. Frederick Kireki ameishukuru Kairuki Hospital Pamoja na mapokezi makubwa waliyoyapata ambapo amesisitiza juu ya kauli mbiu ya “MGONJWA KWANZA” kuwa ni jambo la kujifunza kwani mgonjwa anatakiwa kupewa kipaumbele katika Hospitali yoyote.

Ugeni huo wa siku mbili wa Madaktari wa Magonjwa ya wanawake katika Hospitali ya  Kairuki umepata nafasi ya kujionea Mubashara namna ambavyo mtambo wa Kuondoa Uvimbe bila kufanyiwa Upasuaji unavyofanya kazi ya kutibu mgonjwa.

Aidha, Huduma hiyo ya kuondoa Uvimbe bila kufanyiwa upasuaji inapatikana katika nchi nne Tu Barani Afrika ambapo kwa afrika mashariki na kati inapatikana Kairuki Hospital pekee



Post a Comment

0 Comments