Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cde Ally Hapi (MNEC), anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya siku sita mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha uhai wa Jumuiya na Chama, pamoja na kuendesha mikutano ya hadhara katika wilaya mbalimbali za mkoa huo.
Cde Ally Hapi ataambatana na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji akiwemo Cde Edwin Nyakanyenge kutoka mkoa wa Shinyanga, katika safari yake ya kihistoria ambayo itafanyika wilaya kwa wilaya na jimbo kwa jimbo.
Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili kuwakaribisha viongozi hao na kushiriki kikamilifu katika mikutano itakayofanyika kwenye maeneo watakayopita.
Ziara hiyo itahitimishwa kwa mkutano wa hadhara katika viwanja vya mpira vya Shule ya Msingi Town, kuanzia saa 9:00 jioni Wilaya ya Shinyanga mjini.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka ngazi mbalimbali watashiriki katika mkutano huo, ambapo wananchi wa Shinyanga Mjini wanakaribishwa kwa wingi ili kujadili masuala muhimu yanayohusu jamii.
Wananchi watakaohudhuria mkutano huu watapata fursa ya kuwasilisha kero na changamoto zao, ambapo wataalamu wa serikali walioko pamoja na viongozi wa Chama watakuwepo kutoa majibu na ufafanuzi wa kina kwa kila suala litakalowasilishwa.
Ni nafasi muhimu kwa wananchi kushiriki kikamilifu na kupata ufumbuzi wa matatizo yao moja kwa moja.