Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA DARASA LA SABA: SHULE YA MSINGI LUBAGA YAENDELEA KUNG'ARA KWENYE MATOKEO NAFASI YA KWANZA KIWILAYA KWA MIAKA MITANO MFULULIZO


Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Rose Lesha Rwechongura, akizungumza kwenye mahafali ya 16 katika shule ya msingi Lubaga. 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Rose Lesha Rwechongura, amewahimiza wahitimu wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Lubaga kuwa mfano bora katika jamii na kujiepusha na mienendo mibaya ili kufikia malengo yao.

 Ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya  16 ya shule ya msingi Lubaga, leo Septemba 20, 2024.

Mwalimu Rose amewakumbusha wahitimu umuhimu wa kumweka Mungu mbele katika maisha yao ya kila siku na kuwa kielelezo chema kwa wenzao.

“Ninapenda kuwaasa wanafunzi wahitimu wa darasa la saba  sasa mnatoka mikononi mwa walimu wenu mnaenda katika taasisi ambayo inaitwa Dunia ninaomba mkajitunze, mkajieshimu, mkajisamini utu wenu, ili ninyi mkawe kielelezo kote mnakokwenda muwe na subira na mambo mengine ya kidunia mkamtangulize Mungu kwa mambo yenu yote ili yeye akawategemeze, ili yeye akawaongoze, ili yeye akawaheshimishe, ili yeye akawape yale makusudio ambayo mnayo katika mioyo yenu naimani hapa tutatoa mawaziri hata Rais kwahiyo msikate tama”.amesema Mwalumu Rose

Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga, Mwalimu Stella Lucas Halimoja, amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwa miaka mitano mfululizo, ikishika nafasi ya kwanza kiwilaya kwenye matokeo.

 Mafanikio hayo, amesema, yanatokana na ushirikiano kati ya walimu, bodi ya shule, wazazi, na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na CCM.

“Shule yetu kihistoria ilianzishwa Mwaka 2003 mkapa sasa hii ni mahafali ya 16 tunamshukuru Mungu vijana wetu wanaendelea kufanya vizuri sana na kwa Miaka mitano mfululizo shule yetu imekuwa ikishika nafasi ya kwanza kiwilaya”.

“Maendeleo ya ufaulu wa shule yetu yanatokana na ushirikiano mkubwa tunaopewa na viongozi wetu wa kiserikali na wakichama na viongozi wengine walioko ndani ya kata na hata walioko nje ya kata”.amesema Mwalimu Stella

Diwani wa Kata ya Lubaga, Mhe. Ruben Dotto, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili kuboresha uwezo wao wa kujifunza.

“Niwaombe wazazi kesi kubwa ambayo ni kubwa kuliko kesi zote ni chakula cha watoto shuleni niwaombe wazazi tufanye tufanyavyo tupambaneni kilo moja ya mahindi siyo kitu tutoeni watoto wanywe hata uji lakini kingine mwalimu mkuu wa shule naomba kama kuna watoto wasio weza kabisa kuchangia chakula wawe kumi au 20 tushirikishane”.amesema Mhe. Dotto

Wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Lubaga wamesema wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya taifa waliyofanya mwaka huu 2024.

Jumla ya wanafunzi 65, wakiwemo wavulana 30 na wasichana 35, wamehitimu masomo yao ya darasa la saba 2024 katika Shule ya Msingi Lubaga, Mkoani  Shinyanga.


Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Rose Lesha Rwechongura, akizungumza kwenye mahafali ya 16 katika shule ya msingi Lubaga. 

Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga, Mwalimu Stella Lucas Halimoja, akizungumza kwenye sherehe ya mahafali ya 16 katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga leo Septemba 20,2024.


Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga, Mwalimu Stella Lucas Halimoja, akizungumza kwenye sherehe ya mahafali ya 16 katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga leo Septemba 20,2024.

Wanafunzi wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi Lubaga awali wakiingia ukumbini kwa ajili ya sherehe yao.




 

Post a Comment

0 Comments