MBUNGE IDDI APONGEZA UJENZI WA BARABARA BULYANHULU-KAHAMA

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara inayounganisha Bulyanhulu na Kahama ili kujionea maendeleo ya mradi huo muhimu. 

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Iddi ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa kazi inayofanyika.

Aidha, ametoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuboresha miundombinu nchini, hususan katika jimbo lake la Msalala. Vilevile, amewapongeza wadau mbalimbali, hususan Mgodi wa Bulyanhulu, kwa mchango wao wa kipekee katika kufanikisha ujenzi huo. Pia, hakusita kutoa shukrani kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa usimamizi thabiti na makini wa mradi huu wa barabara.

Ujenzi wa barabara hii unatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa usafiri na uchukuzi kati ya Bulyanhulu na Kahama, hivyo kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi wa maeneo haya.





Previous Post Next Post