MBUNGE IDDI AWAASA UWT KAKOLA KUJIANDISHA KWENYE DAFTARI LA WANACHAMA WA CCM


MBUNGE  wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, amewataka wanawake wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Kijiji cha Kakola, Kata ya Bulyanhulu, kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wanachama cha Mapinduzi (CCM) lengo likiwa ni kujua idadi ya wanachama harisi.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika leo na wanawake wa chama hicho tawi la Kakola, Mheshimiwa Iddi amesisitiza umuhimu wa wanawake kuhamasisha vijana katika jamii zao kujitokeza na kujiandikisha. Alisema kwamba daftari hilo ni nyenzo muhimu kwa maandalizi ya kushiriki kwenye uchaguzi ujao.

"Mkiwa kama wanawake, ni jukumu lenu kuwa mstari wa mbele kuwahimiza vijana wenu na wanajamii kwa ujumla kujitokeza na kujiandikisha, ili waweze kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ambao ni haki yao ya kikatiba na zoezi  la kujiandikisha ni la siku 10 tu," alisema Mbunge Iddi.



Aidha Mbunge Iddi ametumia nafasi hiyo kuwataka wanawake kujitokeza kwa Wingi kuomba nafasi za uongozi ambazo zitatangazwa hili waweze kuchaguliwa pia.

Mbali na hayo, Mbunge Iddi aliwaahidi wanawake wa jimbo hilo kuwa atafanya mkutano na wanawake wote wa Msalala kwa lengo la kusikiliza maoni na mawazo yao kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kimaendeleo.

Habari hii imepokelewa kwa shauku kubwa na wanawake wa kijiji cha Kakola, ambao walionyesha nia ya kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la uandikishaji.
Previous Post Next Post