MR. BLACK (PETER ALEX FRANK) ASHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI KITAIFA MKOANI RUVUMA-SONGEA


Mratibu na muandaaji mkuu wa Tamasha la Utamaduni wa Msukuma Shinyanga (Shinyanga Sukuma Festival) au LEJIGUKULU LYA NZENGO ameshiriki leo tarehe 23/9/2024 kilele cha Tamasha la Utamaduni kitaifa ambalo limefanyika mkoani Ruvuma-Songea huku mgeni rasmi akiwa ni Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mr. Black ameshiriki vyema akiwakilisha tamaduni za msukuma na pia kuendelea kutangaza tamasha la utamaduni wa Msukuma.
 Alipata wasaha pia kukutana na machifu wa sehemu mbalimbali pia viongozi wa serikali na taasisi binafsi.

Mr. Black amesema "Shinyanga naipenda na nitaendelea kuipambania na kuitangaza ulinwenguni kote kupitia utamaduni wake, leo nimeona vingi na hakika Tamasha letu haliko mbali litaongezeka ubora kila siku baada ya siku wana Shinyanga waendelee kutupa support. Sisi kama waandaji kupitia The BSL Investment Company Limited tupo tayari kutangaza utamaduni wa Msukuma"

Chief Kidola wa Shinyanga pia alishiriki vyema kuhakikisha wasukuma hawapoi kitaifa. Nae kaendelea kusisitiza juu ya uendelezaji mila na tamaduni za msukuma kwa manufaa ya taifa endelevu.
















Previous Post Next Post