Na Elizabeth Cornely,SHINYAlNGA
WADAU kutoka mashirika ya Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania(TECMN), umetembelea kituo kinachofanya kazi ya kuokoa, kulea na kuwaendeleza watoto wa kike ambao wamekumbwa na madhila ya ukatili na kukatisha masomo kwa mimba na ndoa za utotoni kilichopo katika Kata ya Chibe wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Wadau kutoka katika mashirika hayo zaidi 80 wamewakilishwa na machache kutoka Msichana Initiative, Medea, Plan International, My Lagacy, Binti Makini Foundation na Theatre Arts Feminist Group, ikiwa ni sehemu ya ziara yao wanayoifanya katika mikoa minne ya Mara, Shinyanga, Tabora na Dodoma.
Mratibu wa Mtandao huo, Lilian Kimati, anasema wameamua kutembelea kituo hicho ili kusikiliza na kushuhudia maisha wanayoishi mabinti hao waliokumbwa na madhila ya ukatili na kuona namna ya kutoa mchango wao.
Mlezi wa kituo hicho kinachojulikana kama Agape Knolwedge Open School, anasema kwa mwaka anapokea wasichana zaidi ya 50 waliopata mimba za utotoni na wale wanaookolewa kwenye ndoa za utotoni.
"Na tukiwaleta hapa, kama walikuwa wanasoma tunafanya mipango wanarudi shuleni na wapo ambao tunawapeleka kujifunza fani mbalimbali za ufundi. Lengo ni kutaka watimize ndoto zao,"anasema Miyola.
"Lakini bado tuna changamoto kubwa sana ya uwezeshaji, asilimia kubwa natoa mfukoni kwangu na ndio maana kuna wakati nikiyumba hali inakuwa mbaya zaidi. Tunaomba kama wapo wadau wanaoweza kutushika mkono waje,"anasema Miyola.
mwisho.
Ofisa Mwandamizi, Kitengo cha Uchechemuzi kutoka Shirika la Msichana Initiative, Lucy Gidamis, akizungumza na mabinti waliokumbwa na madhila ya mimba na ndoa za utotoni kwenye kituo cha Agape