MTOTO WA DARASA LA NNE MWENYE UMRI WA MIAKA 13 ADAIWA KUBAKWA NA JIRANI AKIWA KISIMANI KATA YA CHIBE MANISPAA YA SHINYANGA

Picha ya mtoto mwenye umri wa Miaka 13 mwanafunzi wa shule ya msingi Chibe.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Chibe, inadaiwa kubakwa na Juma Mussa Mmhela anayedhaniwa kuwa na umri wa Miaka 45, mkazi wa kijiji cha Chibe, Manispaa ya Shinyanga.

Tukio hilo linasadikika kutokea Ijumaa, tarehe 16 Agosti 2024, majira ya saa kumi jioni, wakati binti huyo alipokuwa akienda kisimani kuchota maji.

Kwa mujibu wa Mariam Maganga Masabo shangazi wa mtoto huyo, ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Chibe na pia katibu wa Umoja wa Wazazi (UWT) kata ya Chibe ameelezea tukio hilo.

Inadaiwa kuwa, siku hiyo, mtoto huyo alitoka shule na kuelekea kisimani kuchota maji, ambapo Juma Mussa Mmhela alimuona na kumfuata ambapo Juma alimwita mtoto huyo kwa lugha ya Kisukuma, akimshauri kufuata njia nyingine mbali na watoto wengine waliokuwa kisimani baada ya kufika eneo lisilo na watu, Juma alitekeleza kitendo hicho cha kinyama kwa kumvua nguo mtoto huyo na kumfanyia ukatili.

“Siku ya Ijumaa tarehe 16 majira ya saa kumi jioni kuna tukio lilifanywa hapa na baba mmoja anaitwa Juma Mussa Mmhela ambaye alifanya kitendo cha ubakaji wa mtoto wa darasa la nne ambaye anaumri wa Miaka kumi na moja (13) ambaye anasoma shule ya msingi Chibe, siku hiyo binti alitoka shuleni baada ya kula chakula alichukua ndoo na kwenda kwenye maji huyo baba kumbe alimuona wakati anaenda kwenye maji akamfuata alipofika akamwambia nifuate kwa lugha ya kisukuma alipomfuata akamwambia twende huku lakini kwenye maji waliwaacha watoto wezao walipoona wamechelewa kurudi ndiyo wale watoto wakaanza kumtafuta kwenye vichaka badae wakamuona alikuwa amevua chupi na yule baba alikuwa amevua suluali baada ya yule baba kuwaona akainuka na kuanza kuwakimbiza wale watoto”.amesema Mariam

Watoto hao waliporejea majumbani mwao walishindwa kujizuia na kuanza kutoa taarifa kwa familia zao, ingawa mwathirika mwenyewe alikuwa bado anashindwa kuzungumzia tukio hilo hata hivyo, baada ya wazazi wa watoto wengine kupata taarifa hizo, walimtaarifu Mariam Maganga Masabo ambaye alichukua hatua ya kuzungumza na mtoto huyo.

Mtoto alithibitisha kuwa Juma Mussa Mmhela alimbaka na pia alimbaka kwa kumlawiti.

Mariam aliendelea na uchunguzi wa kina na kumuita Juma Mussa kwa mazungumzo, katika mazungumzo hayo, Juma alijaribu kutoa hongo ya shilingi laki tatu ili kuficha ukweli wa tukio hilo, lakini Mariam alikataa na kumtaka Juma akubali kufanyiwa vipimo vya afya.

Wakiwa katika zahanati ya binafsi, polisi walifika na kumkamata Juma, na kisha mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa vipimo zaidi.

Tulikaa kikao nikamwita mtoto akaeleza kweli alimtaja huyo baba, baada ya hapo yule baba akasemaje sasa wewe mama unasema nikamwambia mimi nahitaji huyu binti akapimwe akawa anakataa badae akaniambia twende tukapime kwenye zahanati za watu binafsi lakini pia aliniambia nimsamehe kwamba hatarudia tena alisema anipe laki tatu yaishe nilikataa badae nikamwambia twende kwenye vipimo tukaenda mimi nikawa nawasiliana na polisi wakati tunaendelea na vipimi kwenye hospitali binafsi polisi walikuja kumkamata tukaenda naye kwenye kituo lakini mimi badae nilienda na mtoto kwenda kupima kwenye Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga tulipofika hapo tuliingia wote mtoto alipoanza kukaguliwa na kupimwa kwa kweli inasikitisha walichukua vipimo vyote. amesema Mariam

Mariam Maganga ameiomba serikali ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

 Mwenyekiti wa mtaa wa Chibe, Bwana Kashinje Misana, amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kulaani vikali kitendo hicho akisema, "Hili ni tukio la kikatili na lisilovumilika watoto wetu wanapaswa kulindwa na jamii, siyo kudhulumiwa."

Misalaba Media ilipata fursa ya kuzungumza na viongozi wa jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), wakiwemo katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa Bwana Daniel Kapaya, mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Mwarabu Mwimbili, na katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Bi. Husna Maige.

Viongozi hao wamelani vikali tukio hilo huku wakihimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya sheria katika kutoa taarifa za matukio ya ukatili.

Katika mazungumzo hayo, SMAUJATA imeipongeza serikali kwa hatua ambazo imekuwa ikichukua dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili na kuwakumbusha wananchi kutoa taarifa za matukio kama hayo ili hatua kali zichukuliwe na hivyo kutokomeza ukatili katika jamii.

“Huyu mtoto aliyefanyiwa ukatili anasoma darasa la nne na Mwaka wake huu ni Mwaka wa mitihani kwanza ameathirika kisaikolojia na vilevile ameathirika kimasomo anatakiwa afanye mtihani wake wa taifa sasa hivi yupo tu ametulia kwa sababu ya mtu tu amefanya starehe zake nab ado huyohuyo mtu aliyefanya starehe anamke na watoto saba kwahiyo mimi niiombe sana serikali ya awamu ya siya inayoongozwa na mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wanaohusika hii kesi kwa kweli wasiifumbie macho na sisi tunapaza sauti na tutaendelea kuifuatilia kama SMAUJATA tumeona hapa kuna masuala yalitaka kutembea ya rushwa na huyu mama amekataa rushwa kwa kauli ya SMAUJATA tunatoa kauli moja kuwa hii kesi isichukue muda na tunaomba hii kesi ifike mahakamani moja kwa moja huyu mtu achukue adhabu yake ya Miaka 30”.amesema katibu wa SMAUJATA kanda ya ziwa Bwana Daniel Kapaya

Viongozi wa jumuiya ya SMAUJATA wakiwa na Mariam Maganga Masabo shangazi wa mtoto huyo, ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Chibe na pia katibu wa Umoja wa Wazazi (UWT) kata ya Chibe. 


Previous Post Next Post