Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING: MWANAUME AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwanaume mmoja aitwaye Charles Kastory Kashinje, mwenye umri wa miaka 24 na mkazi wa kijiji cha Idodoma, kata ya Samuye, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amekutwa ameuawa kwa kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake kando ya barabara.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumatatu, Septemba 9, 2024.

Misalaba Media imefanya mahojiano na Mwenyekiti wa kijiji cha Idodoma, Bwana Masesa Izengo Chaba ambaye ameeleza jinsi alivyopokea taarifa hizo.

“Nilipewa taarifa saa mbili asubuhi kwamba kijana mmoja ameuawa kwa kukatwa mapanga na kuchinjwa, marehemu ni dereva wa bodaboda na alikuwa anaishi na baba yake, akiwa na mke na watoto wawili wa kike, mwili wake ulikutwa jirani na mto wa Idodoma, umelazwa kwenye pikipiki yake baadaye polisi walikuja wakauona huo mwili badaye wakaruhusu kuendelea na taratibu za mazishi kwahiyo tayari jioni ya leo amezikwa”.amesema Mwenyekiti Chaba

Diwani wa viti maalum kata ya Samuye, Mhe. Leticia Masalu naye ameongelea tukio hilo.

“Na mimi nilipigiwa tu simu asubuhi nikaambiwa kuna mtu ameuawa yaani amechinjwa wamemkuta tu eneo la Idodoma lakini kuna poli eneo hilo nyumba zipo mbali, kweli nimefika kwenye eneo la tukio nikaona, niwaombe tu wananchi tuwe makini maana hili limekuwa ni janga kubwa sana tuzingatie usalama wetu hasa inapofika usiku tusitembee peke”.amesema Mhe. Leticia

Misalaba Media inaendelea kufuatilia taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika, ikiwemo Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ili kupata maelezo ya kina kuhusu tukio hilo na hatua zinazochukuliwa.

Post a Comment

0 Comments