Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA, JOHN MONGELLA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI, WAJUMBE WA BARAZA LA JUMUIYA NA MABALOZI

Na Mapuli Kitina Misalaba
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, leo Septemba 6,2024 amezungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, wajumbe wa baraza la jumuiya na mabalozi katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa idara katika Manispaa ya Shinyanga.

Mongella ameanza ziara ya siku saba mkoani Shinyanga, yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2024 na kuimarisha uhai wa chama ambapo atafanya mikutano ya hadhara na ya ndani ili kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa Shinyanga.

Ziara hiyo itamfikisha katika maeneo mbalimbali ikiwemo Shinyanga Vijijini, Kahama, Msalala, Kishapu, na Ushetu ambapo atakutana na viongozi wa chama na wananchi kujadili namna bora ya kuimarisha utekelezaji wa sera za chama kwa maendeleo ya mkoa.  

Aidha, ziara hii inalenga kuwahamasisha wanachama wa CCM kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama na kushughulikia kero za wananchi. 

Leo, Mongella atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa shule ya msingi Town, Manispaa ya Shinyanga, ambapo anatarajiwa kuzungumza na wananchi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mkoa.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, akizungumza  na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, wajumbe wa baraza la jumuiya na mabalozi katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Septemba 6,2024.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano huo leo Septemba 6,2024.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano huo leo Septemba 6,2024.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mkutano huo leo Septemba 6,2024.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Hamisa Chacha akitoa utambulisho kwenye mkutano huo leo Septemba 6,2024.

Katibu mwenyezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Said Bwanga awali akitoa utambulisho wa viongozi na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo leo Septemba 6,2024.

Katibu mwenyezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Said Bwanga awali akitoa utambulisho wa viongozi na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo leo Septemba 6,2024.

Mkutano wa  wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, wajumbe wa baraza la jumuiya na mabalozi ukiendelea katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Septemba 6,2024.

Tazama picha za matukio mbalimbali wakati wa mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, Mkoani Shinyanga leo Septemba 6,2024.

Post a Comment

0 Comments