Ameandika Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Ukurasa wake Mtandao wa X
"Ahsanteni sana Tunduru.
Tuendelee kufanya kazi na kuinuka kiuchumi kupitia fursa zinazoletwa na ujenzi wa miundombinu mipya, uboreshaji wa afya, elimu, kuongezeka kwa ruzuku katika kilimo, masoko, afya, maji, uwekezaji kwenye sekta ya madini na msingi wa amani na utulivu tulio nao.
Katika kuendelea kufufua viwanda vyetu, nimeiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kuhakikisha inakifufua kiwanda cha kubangua korosho wilayani Tunduru ambacho mwekezaji aliyebinafsishiwa ameshindwa kukiendesha. Kiwanda hiki kirudi tena kufanya kazi na kurejesha ajira na fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma".