SERIKALI YADHAMILIA KULIBADILI JESHI LA POLISI












Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Omar Issa akiapa mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa kofia) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ally Senga Gugu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe na Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu(wapili kulia),Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Omar Issa(wakwanza kushoto),Katibu wa Bodi hiyo,Dkt.Prosper Kiramuu(kulia) na wajumbe na watendaji wa bodi na shirika hilo baada ya Hafla ya Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Katibu wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi,Dkt.Prosper Kiramuu akiapa mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa kofia) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Ally Senga Gugu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu akizungumza na Wajumbe na Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika Makao Makuu ya wizara jijini Dar es Salaam.Jumla ya wajumbe tisa waliapa kuhudumu katika bodi hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amezindua Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi huku akiipa majukumu bodi hiyo kulisimamia shirika ambalo linaenda kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa kutumia dhana za teknolojia ya kisasa ili kuweza kustawisha amani na utulivu kwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.


Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Omar Issa ambae alikua Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kufuatilia Mfumo na Utendaji wa Taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi,Magereza,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya.


‘Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi sasa huwezi kuwa na Jeshi la Polisi la kisasa ambalo linafanya kazi kutumia mifumo ya zamani ndio maana tunazungumzia upelekaji wa jeshi kwenye ngazi za kata na uwepo wa ofisi bora na za kisasa tukiamini uhalifu unaanzia chini,wote tumeshuhudia changamoto kubwa sana ya uhalifu uliokithiri katika nchi hii ukihusisha viungo vya watoto wadogo ili mtu apate utajiri vitu ambavyo vinaleta uhalifu katika jamii sasa katika kulipa uwezo jeshi letu kupitia Shirika la Uzalishaji Mali katika kujenga vituo na kusimamia miradi mikubwa ikiwemo mradi wa miji salama tunaiomba bodi sasa ilisimamie shirika ili lipate kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa ili hatimaye tudhibiti masuala ya uhalifu kwa njia za kisasa’alisema Masauni


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu amesema wizara iko tayari kutoa ushirikiano kwa shirika na bodi pamoja na kusimamia mambo ya kisera ili azma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya jeshi letu kuwa la kisasa zaidi.


‘Mimi kama mtendaji mkuu wa wizara nimesimama kuwahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano wowote mtakaohitaji kutoka kwa wizara najua majukumu yenu yatatuhitaji kwa kiasi kikubwa ili kupata miongozo ya kisera ili muweze kutimiza shughuli za kiutendaji na matarajio ya wizara kwenye shirika letu ni makubwa na kuna matarajio mengi ya kufanya mabadiliko makubwa’ alisema Katibu Mkuu


Wakizungumza kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi,Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Omar Issa na Katibu wa bodi hiyo,Dkt.Prosper Kiramuu waliishukuru serikali kwa kuwaamini na kuhaidi kutimiza malengo ya serikali yaliyokusudiwa kupitia shirika hilo.
Previous Post Next Post