SHINYANGA: KAMISHNA WA KODI ZA NDANI KUTOKA TRA ASISITIZA USAWA KATIKA ULIPAJI WA KODI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Alfred Mrengi, amesisitiza dhamira ya mamlaka hiyo kuendelea kusimamia usawa katika ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara.

Akizungumza katika kikao cha pamoja na wafanyabiashara kilichofanyika leo Septemba 25, 2024 mjini Shinyanga, Bwana Mrengi ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara analipa kodi kulingana na uwezo na ukubwa wa biashara yake.

"Tutaendelea kusimamia usawa katika ulipaji wa kodi mfanyabiashara mkubwa atapaswa kulipa kodi kubwa kulingana na biashara yake, na mfanyabiashara mdogo naye atalipa kodi kidogo kulingana na hali halisi ya biashara yake," amesema Bwana Mrengi.

Ameongeza kuwa si jambo linalokubalika kuona mfanyabiashara mkubwa akilipa kodi ndogo kuliko mfanyabiashara mdogo ambapo ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kulipa kodi kwa wakati na kwa kiasi kinachostahili, huku akisisitiza kwamba TRA ni taasisi rafiki inayopaswa kushirikiana na wafanyabiashara katika kutatua changamoto za kibiashara.

"Tutaendelea kutoa maamuzi yetu kwa kuzingatia weledi bila kuvunja matakwa ya kiserikali pia, hakuna mtumishi wa TRA aliye juu ya sheria, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa huduma zetu zinatolewa kwa uadilifu na kwa kuzingatia taratibu zilizopo,"amesema Mrengi.

Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bwana Josephat Mwaipaja, amewakumbusha wafanyabiashara kutumia siku ya Alhamisi, iliyotengwa rasmi kusikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara, ili kutafuta suluhisho kwa pamoja.

Katika kikao hicho, watumishi wa TRA wamekumbushwa kuweka utaratibu wa kuwatembelea wafanyabiashara mara kwa mara ili kuboresha huduma.

Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga Hatibu Mgeja, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya TRA na wafanyabiashara kwa ustawi wa biashara na uchumi wa mkoa huo.

Kikao hicho kimejenga uelewa mkubwa kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kushirikiana na mamlaka hiyo kwa maendeleo endelevu ambapo wafanyabiashara wameuliza maswa na kutoa maoni kuhusu namna bora ya kulipa kodi.

Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Alfred Mrengi, akizungumza kwenye kikao cha pamoja na wafanyabiashara Mkoani Shinyanga Septemba 25, 2024.

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bwana Josephat Mwaipaja, akiwaomba wafanyabiashara kupeleka changamoto zao ili ziweze kutatuliwa haraka.

Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Bwana Josephat Mwaipaja, akiwaomba wafanyabiashara kupeleka changamoto zao ili ziweze kutatuliwa haraka.

Previous Post Next Post