Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka
75, mkazi wa kijiji cha Masengwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amefariki
dunia ndani ya chumba chake baada ya kudaiwa kumeza vidonge vinavyosadikika
kuwa vya sumu ya panya.
Tukio hili
limetokea mnamo Septemba 22, 2024, majira ya asubuhi.
Misalaba Media imezungumza na mwenyekiti wa kijiji
cha Masengwa Bwana Zachalia Ntemi Sanane, ambaye alielezea jinsi alivyopokea
taarifa ya tukio hilo.
Sanane alieleza kuwa baada ya kufika kwenye familia
hiyo, alimjulisha mtendaji wa kijiji, ambaye naye alimuarifu mtendaji wa kata
ili kuwaita polisi.
Polisi walifika eneo hilo saa kumi na moja jioni
wakiwa na daktari wao. Baada ya kuchukua maelezo kutoka kwa familia na kukagua
masalia ya vidonge, waliwaruhusu waendelee na taratibu za mazishi.
“Nilitoka
kanisani muda wa mchana badae nikapigiwa simu kwamba sogea hapa kwenye familia
ya Suzana Jinya Ganai kweli nilienda kufika pale nikamkuta mama yule tayaru
mauni yamemkuta”.
“Baada
ya kufika katika familia hiyo nilimpigia mtendaji wangu wa kijiji nikamwambia na yeye akasema ampigie mtendaji
wa kata ili awapigie polisi wakati wanakuja mimi nilianza kuchukua maelezo
kwenye familia wakasema mama huyo hakuwa na ugomvi na mtu yoyote maana anaishi
yeye, mama yake mzazi, watoto na wajukuu wake ambapo asubuhi siku ya Jumapili
watoto wote aliwaambiwa waende kanisani baada ya watoto hao kwenda kanisani
kumbe yeye alikuwa amepanga sasa kufanya maamuzi hayo inasemekana alikunywa
dawa ya panya alimeza vidonge viwili kimoja alikitapika walikikuta chini”.
“Badae
polisi walikuna muda wa saa kumi na moja walikuwa na daktari wao wakapinga na
wao walichukua maelezo kwa familia walienda kuangalia alipotapika wakaona
masalia ya vidonge badae wakaturuhusu kuendelea na taratibu za mazishi”.amesema
Sanane
Mazishi ya Suzana Jinya yamefanyika leo saa nane
mchana katika kijiji cha Masengwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Misalaba Media inaendelea kumtafuta kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa zaidi kuhusu upelelezi wa tukio hilo.