CARITAS TABORA YATOA VYEREHANI VYA ZAIDI YA M.17 KUSAIDIA WANAWAKE VIJIJINI

Mkurugenzi wa CARITAS Tabora Padri Paschal Kitambi akikabidhi cherehani kwa kikundi cha wanawake ‘Single mother’

Na Lucas Raphael ,Tabora

Shirika la maendeleo la Kanisa Katoliki mkoani Tabora CARITAS limetoa vyerehani 54   kwa wanawake ‘Walea Pweke’ wa Vijiji vya wilaya ya Uyui Mkoani humo kwa lengo la kuonyesha upendo kwao na kuwakwamua kiuchumi vyenye thamani ya sh.milioni 17,820,000.

 

Akikabidhi vyerehani hivyo jana mkurugenzi wa CARITAS Mkoani hapa, Padri Paschal Kitambi  kwa wanawake hao ‘Single mother’ katika Kata ya Isikizya wilayani Uyui  alisema kuwa lengo la msaada huo ni kuonyesha upendo wao  kwa vitendo  na kuwakwamua kimaisha.

 

Alisema kuwa idara hiyo imewashika mkono akinamama hao ambapo nao wanatakiwa kuinuka na kuendeleza jitihada za kujipatia vipato,kujiimarisha kiuchumi na hatimaye kujiletea maendeleo yao na kuwa mfano bora kwa jamii.

 

‘CARITAS imewashika mkono na mkumbuke Kanisa linasisitiza upendo kupitia salamu ama kauli mbiu yetu ya dini mbalimbali,upendo na amani,hivyo na nyie msimame msonge mbele na kuonyesha upendo huo kwa wengine kwa kufanya maendeleo makubwa zaidi ya haya’alisema.

 

Makamu Mwenyekiti wa kikundi cha Tunda Jema Mwajuma Jumanne akisoma risala yao alisema kuwa wana vikundi 10 vilivyo jumla ya wanachama 124 waliopatiwa mafunzo ya ujasiriamali na masuala ya kuweka na kukopo SACCOS ambapo wamfanikiwa kupata uelewa wa kutosha.

 

Alisema CARITAS iliwawezesha shilingi .500,000 kila kikundi ambapo waliweza kukopeshana na kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia vipato vya kuendesha maisha yao na waliiomba idara hiyo kupanua wigo wa mafunzo wanayowapa kwa kuwapeleka nje ya wilaya hiyo kwenda kujifunza na kubadilisha ujuzi na watu wa maeneo mengine.

 

Hawa John (26) mkazi wa Kata ya Ilolwansimba na  Sada Maasudi (28) wa Kata ya Isikizya walisema kuwa vyerehani hivyo walivyopewa na CARITAS vitawasaidia kuwapatia vipato vyao na kwamba idara hiyo imewawezesha kujiunga katika vikundi na kupta elimu ya VICOBA vinavyowasaidia kukopeshana na kuinua hali ya uchumi wa familia zao.

Mratibu wa mradi huo wa kuwawezesha wanawake hao Haruna Nelson alisema kuwa CARITAS ilitoa vyerehani hivyo ambapo kila kimoja kinathamani ya sh.330,000 na kwamba wamewapa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuwapatia watoto wao sare za shule.

 

Nelson alisema kuwa idara yao ikiwa chini ya Kanisa hilo inasisitiza suala la upendo katika jamii na kusaidiana bila kujali ama kubagua kwa itikadi ya dini,kabila au muonekana wa mtu na kwamba imewasaidia wanawake hao ambao wapo walioachwa na wenzi wao kwa kutelekezwa na kufariki dunia.

 

Aliwahimiza wanawake wengine wajiunge katika vikundi vitavyoratibiwa na CARITAS ambapo watapatiwa mafunzo na kuwezeshwa na watajihakikishia maendeleo ya uhakika na kuwa na maisha bora wao pamoja na familia zao na taifa kwa ujumla  .

MWISHO.

Ni kinamama wa wilayani Uyui wakiwa Katani Isikizya wakati wa ugawaji wa vyerehani

Previous Post Next Post