Na Bora Mustafa,
Misalaba Media,
Arusha.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)imetoa elimu kuhusu masuala ya Rushwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwakani .
TAKUKURU imetoa elimu hiyo kwa Wanahabari ikiwa imebakia miezi kadhaa hadi kufikia Novemba 27 ambapo Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo amesema kuwa Taasisi inafanya wajibu wa kuelimisha umma kupitia vyombo vya habari lengo kuwaelimisha wananchi kuwa wanawajibu wa kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi .
Pia amesema kuwa Taasisi inawajibu wa kuchunguza vitendo vya rushwa kwanzia wakati wa uandikishwaji wa daftari, kampeni na uchaguzi na kuwataka wananchi kuripoti vitendo vya rushwa mahala husika ili hatua za kisheria zichukuliwa.
"Wananchi wanatakiwa watoe ushirikiano wa kutosha siyo kwa kutoa tu taarifa bali na kutoa ushahidi wa nyaraka au wa kuongea na mtu huyo atalindwaa ili asipate hofu juu ya usalama wake" amesema Ngailo
Kwa upande wao waandishi wa habari wameitaka Taasisi hiyo kuhakikisha haki inatendeka bila kuendelea chama chochote cha siasa ili mwananchi aweze kupata
"Ili mwananchi aweze kujitokeza kupiga kura ni wajibu wenu kumhakikishia kuwa kura yake itaenda kihalali, na siyo kupiga kura na matokeo yawe ndivyo siyo, kwa hiyo elimu hii kwetu itaenda kuwaondoa hofu wananchi, hivyo na ninyi mhakikishe mtalinda kura yake" amesema Claud Gwandu, Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC).