VIJANA WA BODABODA 180 WA BUKOBA MJINI WALIPIWA MAFUNZO YA UDEREVA

Shirika la Omuka Hub lililo chini ya Mhe Neema Lugangira ambae  ni Mlezi wa Chama cha Madereva wa Pikipiki na Wamiliki  Bukoba Mjini

wamezindua Kozi Namba 1 ya Usalama Barabarani ambapo Bodaboda 180 watapata mafunzo ya udereva na cheti bure ili waweze kupata leseni na gharama zote zimelipiwa na Omuka Hub ambayo pia itachangia nusu ya gharama ya leseni.

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Kozi hiyo alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera (RPC) ACP Yusuph Daniel.

Lengo la Omuka Hub ni kuwafikia wanachama wote katika Chama Cha Madereva wa Pikipiki na Wamiliki kwa Bukoba Mjini awamu moja baada ya nyingine kwa lengo la kuimarisha usalama barabarani, kupunguza ajali, kuokoa maisha pamoja na kuwaunganisha vijana  na fursa mbalimbali. 

Aidha, katika Uzinduzi, Vijana wa Bodaboda walipokea elimu kuhusu fursa za kujiunga na NSSF na walianza kujisajili.










Previous Post Next Post