Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WALIA NA DEMOKRASIA HURU NCHINI

Na Bora mustafa, Misalaba Media, Arusha .

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt Benson Bagonza ameitaka serikali kuweka mazingira bora yatakayowapa wananchi kupata uhuru wa kidemokria.

Akizungumza katika kilele Cha wiki ya AZAKI Dkt Bagonza amesema Taifa limeingia katika Giza kwa sababu ya kutokuwa na Demokrasia ya kweli ,hivyo amewahimiza wananchi kupambana Ili kuwa na uongozi bora utakao leta manufaa na tija katika
 Taifa.

 Amesema katika katiba yetu haiaangalii kundi wala udini ili mtu aweze kuwa Kiongozi hivyo kila mtu ana haki ya kuchaguliwa.

Askofu amesema tuliingia katika mfumo wa vyama vyingi tukijua tutaweka usawa kwa jamii lakini haikuwa hivyo na hatuwezi kurud kwenye mfumo wa chama kimoja.

"Mfumo wa Demokrasia tulio nao ni huu ambao tuna uhuru wa kupiga kura na sio kuchagua ,mfumo unaoruhusu Udikteta, ni mfumo unaoruhusu mawazo na sio kumuhakikishia ulinzi na chama chake, na ni mfumo unaoruhusu mashaka ya kudumu kwa wote" amesema Dkt Bagonza.

Amesema zipo sababu mbali mbali ambazo zinathibitisha kuwa hakuna Demokrasia katika nchi yetu ikiwemo kutokuwa na uhuru wa vyombo vya habari,hakuna uhuru wa kukusanyika pamoja na kuongezeka kwa Rushwa .


Pia amesema Kuna changamoto mbalimbali ambazo zinadidimiza kutokuwepo kwa Demokrasia ya kweli katika nchi kwa kukosekana kwa kundi linalowaza kuunganisha vyama vyote viwe kitu kimoja.

"Hapa tulipofikia kuna kundi linalotamani chama Tawala kisambaratike, lipo kundi linalotamani vyama vyote visambaratike" amesema

Aidha amesema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliasisi siasa ya 4R lakini ukichunguza kwa makini huwezi kuacha kuona Taifa lipo gizani na mfumo huu unategemea sana hekima ya mtu binafsi kuliko mfumo wenyewe.
 
Hata hivyo amesema Ili tuwe na Demokrasia ya kweli inabidi tuwe na Uongozi imara na Taasisi zake .

Kwa upande wake Rais wa AZAKI Dr.Stigmata Tenga amesema inabidi tutoe matabaka kati ya wananchi na Serikali Ili tupate maendeleo.

"Inabidi wadau wazingatie mambo matatu ambayo ni uongozi bora ambao utaleta chachu ya maendeleo katika jamii, pili wananchi washirikiane katika kazi za kuendeleza jamii kimaendeleo na tatu tuangalia mfumo unaokandamiza wananchi katika Jamii yetu.....hivyo tuongee na kupaza Sauti" amesema Dkt Tenga.



Post a Comment

0 Comments