Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne maarufu ‘waliotumwa na afande’, baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.

Ni katika kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 iliyokuwa inawakabili washtakiwa hao akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024. Pia, Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya Sh1 milioni.

Soma hapa zaidi chanzo.Mwananchi