Na. Mwandishi wetu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura mkoani Mara, Simiyu na baadhi ya halmashauri za mkoa wa Manyara utafanyika
kwa siku saba kuanzia kesho tarehe 04 hadi 10 Septemba, 2024 ambapo jumla ya
wapiga kura wapya 491,050 wanatarajiwa kuandikishwa. Kwa mujibu wa makadirio yaliyofanywa na Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi na ambayo yanatokana na takwimu za Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka 2022, idadi ya wapiga kura 3,391,017 wanatarajiwa kuwemo kwenye
Daftari la Kudumumu la Wapiga Kura kwenye mikoa hiyo wakati wa uchaguzi mkuu wa
mwaka 2025. Hata hivyo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan idadi hiyo
inaweza kuongezeka zaidi. “Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa
inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga
kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au
nyingine hawakuweza kujiandikisha kuwa wapiga kura,” amesema Bw. Kailima. Kwenye uboreshaji huo wa Daftari jumla ya
vituo 4,373 vitatumika kuwaandikisha wapiga kura wapya na kuboresha taarifa za
wapiga kura walioandikishwa kwa miaka iliyopita. Uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hiyo
unafanyika ikiwa ni mwendelezo wa zoezi hilo lililozinduliwa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa Majaliwa mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 ambapo mzunguko wa
kwanza ulijumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora. Baada ya uboreshaji kukamilika kwenye mikoa
hiyo ulifuata mzunguko wa pili kwenye mikoa ya Kagera na Geita na wa tatu
kwenye mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Mzunguko wa nne wa uboreshaji wa Daftari
unajumuisha mkoa wa Mara, baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Manyara ambazo ni
Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang na
Mbulu na mkoa wa Simiyu ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00
asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Tunapokea watoto kwa ajili ya Nursery na Primary kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Ada kwa Muhula:
- Nursery: 150,000/=
- Primary: 210,000/=
Usafiri na hosteli zinapatikana.
Shule ipo Basihaya-Dawasco.
Mawasiliano:
0714 927 246
0766 927 247
Nafasi ni chache sana!
ADSTERRA
OFA KUBWA YA MAFUNZO YA UOKAJI BIASHARA MWANZA NA KANDA YA ZIWA
WASILIANA NASI 0788 774 594 au 0715 224 264
OFISI YA MARIASUZY BAKERY EXPERT (SME)
Inakuletea OFA KUBWA ya mafunzo ya uokaji na uendeshaji wa biashara kwa mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa.
Mafunzo haya yanalenga kukupa ujuzi na mbinu bora za uokaji pamoja na usimamizi wa biashara zako ili kuhakikisha unafanikiwa katika sekta ya ujasiriamali.
Tarehe: Kuanzia 28 Oktoba 2024 hadi 1 Novemba 2024
Muda: Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni
Mahali: Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza
Ada:Shilingi 125,000 kwa siku 5
Malipo: Yafanyike kupitia akaunti ya Azania Bank, A/C: 001810427389 – Mary Malemi.
NB: Nafasi 10 za bure zinatolewa kwa walemavu.
Kwa mawasiliano zaidi:
Simu: 0788 774 594 au 0715 224 264
Usikose nafasi hii ya kipekee ya kuongeza ujuzi wako na kuimarisha biashara yako!
0 Comments