WATUMIA BURUDANI KUTOA ELIMU KUPAMBANA NA UKATILI/ NDOA ZA UTOTONI


Na Elizabeth Cornely
WADAU wa Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania(TECMN), umeendelea na ziara yake wilayani Nzega mkoani Tabora kwa kutoa elimu ya namna ya kupambana na ukatili pamoja na ndoa za utotoni.

Mtandao huo unaoundwa na mashirika zaidi ya 80, katika ziara hiyo unawakilishwa na machache ikiwamo Msichana Initiative, Binti Makini Foundation, Theatre Arts Feminist Group, Medea Tanzania, Plan International na My Legacy.


Katika kijiji cha Isagenhe wilayani humo, wadau wa mtandao huo waliendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwamo kwa kutumia nyimbo na burudani kwa lugha asili ya wakazi wa eneo hilo.

Wadau hao wanafanya ziara ya kutoa elimu ya kupambana na ukatili na ndoa hizo za utotoni kwa mikoa ya Mara, Shinyanga, Tabora na Dodoma ambayo kwa takwimu inaonyesha iko juu katika ndoa hizo za utotoni.


Kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa Demografia na Afya(TDHS) za mwaka 2015/2016, asilimia 36 ya wasichana Tanzania wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 huku mikoa kinara kwa ndoa hizo za utotoni ni Shinyanga asilimia 59, Tabora asilimia 58, Mara 55 na Dodoma ni asilimia 51.


mwisho.





Baadhi ya wadau wa Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania(waliovalia tisheti nyeupe na kofia) wakiungana na kikundi cha burudani cha kijiji cha Isagenhe kucheza ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili na ndoa za utotoni nchini

Previous Post Next Post