WAZIRI, PINDI CHANA AOMBA MACHIFU KUHUBIRI UMOJA NA AMANI KUELEKEA CHAGUZI

Na Elizabeth Cornely

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amewaomba Machifu kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhubiri umoja, amani na mshikamano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Waziri Chana ametoa kauli hiyo mjini Songea alipozungumza na Machifu hao walioshiriki katika Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalohitishwa leo mkoani Ruvuma.

Amesema viongozi hao wa kimila wana mchango na nguvu kubwa ya kuhubiri umoja na amani kwa wananchi wao hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye chaguzi.

"Leo hii nchi yetu ina utulivu na amani kwa sababu miongoni mwa watu waliochangia kufanikisha hilo ni Machifu pamoja na viongozi wa dini, tunaomba muendelee kufundisha kizazi cha sasa na kijacho mila na desturi za nchi yetu,"amesema Waziri Chana.

"Tukumbuke tuko kwenye maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, kwa hiyo kwanza tuhamasishe watu wagombee lakini kulinda umoja na amani ya nchi yetu."

Mwisho.

Previous Post Next Post