Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA VIWANDA SELEMAN JAFO AKIZINDUA MAONESHO YA CHEMBA YA WAFANYABIASHARA MWANZA



WAZIRI wa Viwanda na Biashara Seleman Jaffo ameitaka chemba ya Biashara, Vwanda na Kilimo (TCCIA) kuanza maonesho hayo kwa ngazi ya kitaifa kwa bidhaa na huduma wanazozalisha ndani ya Afrika Mashariki.

Jaffo alisema hayo Jana Jijini Mwanza katika uzinduzi wa maonesho ya 19 ya TCCIA ambapo wadau mbalimbali toka Jukwaa la Biashara, Viwanda na Kilimo wa eneo lote la Afrika Mashariki.

 Alisema maonesho hayo yana tija zinazowawezesha wadau hao kubadilishana uzoefu, maarifa na kujenga mahusiano ya watu wa ukanda wa Afrika Mashariki kuwa na nguvu.

"Natamani kusikia wafanyabiashara toka mataifa mengine hawarudi na bidhaa zao kwani hapa nchini kuna soko la vitu hivyo muwe na mikataba ya kibiashara"alisema Jaffo.

Jaffo hatua ya kuimarisha mashirikiano itawawezesha kufanya biashara hata kupitia Mpango wa Kukuza na kuongeza Fursa (AGOA) unaoruhusu bidhaa mbalimbali kuingia bila vikwazo nchini Marekani na soko la Afrika.

Naye Makamu wa rais wa TCCIA Boniface Ndengo pamoja na kupongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha ulinzi wa mitaji yao chini sera nzuri aliomba iharakishwe jitihada ya kuwepo kwa mazingira rahisi ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Alisema wanadhamiria ya kuuza bidhaa zao katika soko la Afrika hivyo mazingira ya ulipaji kodi yaongeze kasi ya wafanyabiashara kutokuwa waoga kufanya biashara kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.

Naye Mkrugenzi Mtendaji wa Mohpans Herbal Medicine & Nutritional Supplements Prof Wanfoko Henry toka nchini Uganda mshindi kwenye maonesho hayo, alisema anashukuru kuwepo kwa tukio hilo kwani inawapa fursa ya kuuza bidhaa zao za dawa katika soko hilo na kusaidia kufundisha utengenezaji wa dawa.

Alisema tiba Asili ina umuhimu kwa waafrika kwani inasaidia kuponesha magonjwa mbalimbali ambayo yanawafanya watu kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali katika maeneo yao.

Hilda Massam wa PH Selection mshindi wa maonesho hayo toka nchini Tanzania alisema tiba Asili wanazozalisha zinasaidia katika kufanya ngozi kurudia katika ubora wake wa awali.

Alisema fursa hiyo ya biashara na mataifa ya Afrika Mashariki inawasaidia vilevile kujua ubora wa dawa wanazotengeneza hapa nchini.

Teddy Mkami Mkrugenzi Mtendaji TJM Product mshindi wa tuzo hizo toka Tanzania mkazi wa Jijini Mwanza, alisema anatamani kauli mbiu ingekuwa "Afrika Tunaweza" anasema dawa zake ambazo tiba lishe zinaonesha mafanikio makubwa.

Alisema dawa za kiafrika zina matokeo chanya na hilo limejidhihirisha kipindi Cha UVIKO19.



Post a Comment

0 Comments