ASA KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO HADI KUFIKIA TANI 8,568

Kaimu mkurungezi mtendaji wa Wakala wa Mbegu za kilimo ( ASA), Leo Mavika  akizungumza  wakati akifunga mafunzo ya  Siku tatu ya Technolojia za Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo kwa watumishi wa ASA


Na Lucas Raphael,Tabora

Wakala wa Mbegu za kilimo ( ASA) Unatarajia kuongeza uzalisha wa Mbegu bora za  kilimo kutoka tani 5,000 hadi kufikia Tani 8,568 kwa msimu wa Kilimo 2024/2025.

  

Kauli hiyo ilitolewa na kaimu mkurungezi mtendaji wa ASA , Leo Mavika   wakati akifunga mafunzo ya  Siku tatu ya  Technolojia za Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo kwa watumishi wa ASA Mkoani Dodoma kupitia programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi - AFDP.

 

Alibainisha kuwa kutolewa kwa Mafunzo hayo ni maandalizi ya kuongeza Uzalishaji wa Mbegu kutoka Tani 5,000 hadi kufikia Tani 8,568 kwa mwaka wa Kilimo 2024/2025.

 

Alifafanua kwamba ongezeko la Uzalishaji kwa Mazao kama vile Mahindi yatazalishwa tani 2,412, Alizeti tani 120, Maharage tani 500, Choroko tani 30, mboga mboga tani 6, Ngano tani 1,500, Soya tani 200, Mpunga tani 1,200, Mtama tani 400 pamoja na Ufuta tani 150.

 

Mavika alisema ASA imeweka mikakati mizuri ya kuhakikisha inaongeza Uzalishaji mkubwa ilikufikia Malengo ya serikali yaliyopangwa.

 

Aidha aliongeza kuwa Wakala wa Mbegu ina rasilimali ardhi ya kutosha hivyo ina kila sababu ya kuongeza Uzalishaji usiokuwa na shaka kwa maslahi ya Taifa.

 

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Wakala wa Mbegu, Angolile Mbugi alisema Mafunzo hayo yataleta mabadiliko makubwa kwa Taasisi hasa katika sekta ya Uzalishaji.

 

Aliwataka watumishi wote wa Wakala kuwa waadilifu katika uwajibikaji wao pamoja na kuepuka vishawishi vyote vinavyoweza kuhalibu taswira ya Wakala.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzalishaji Dkt, Justin Ringo alisema maelekezo yote yaliyotolewa na kaimu Mtendaji Mkuu yatafanyiwa kazi kulingana na uzito wake.

 

Alisema kwamba  watumishi wote kuzingatia mafunzo yaliyotolewa na wawezeshaji kwa muda wote wa siku tatu ili kuongeza Uzalishaji wenye tija kwa Taasisi.


Watumishi wakala wa Mbegu za kilimo ( ASA),wakiwafuatilia watoa mada juu ya  wote kuzingatia mafunzo Technolojia za Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo

Previous Post Next Post