Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho Jumatano tarehe 16.10.2024, atafanya ziara ya kichungaji ya siku moja katika Parokia ya Wila wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa Paroko wa Parokia ya Wila Padre John Nkinga, Askofu Sangu atapokelewa Parokia ni Wila majira ya saa 2:00 asubuhi, ambapo pamoja na mambo mengine, ataweka jiwe la msingi katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu senta ya Mwamashele na kupokea taarifa ya Kanisa hilo, ambalo linapendekezwa na waamini wa senta hiyo kuwa Parokia teule.
Baada ya zoezi hilo, Askofu Sangu atarudi makao makuu ya Parokia ya Wila kwa ajili ya adhimisho la Misa takatifu ambayo itaanza saa 4:00 asubuhi, itakayokwenda pamoja na utolewaji wa Sakramenti ya kipaimara kwa waimarishwa wapatao 170.
Kupitia ziara hiyo, Askofu Sangu pia atakabidhiwa zawadi na michango mbalimbali kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa na atashiriki sherehe fupi itakayowashirikisha waamini na watu mbalimbali wanaoizunguka Prokia ya Wila (wanazengo)