CCM KATA YA NDEMBEZI YAONYESHA IMANI KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI, WAGOMBEA WOTE MITAA SITA WARUDISHA FOMU

Na Mapuli Kitina Misalaba

Katika kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Ndembezi Jimbo la Shinyanga Mjini, kimetumia fursa hii kupongeza ushirikiano na uwazi wa wasimamizi wa serikali katika zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za wagombea.

Akizungumza na Misalaba Media baada ya zoezi la kurejesha fomu, Katibu wa CCM wa Kata ya Ndembezi Pendo John Sawa, ameeleza kuwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu limekwenda kwa utaratibu mzuri huku wasimamizi wa uchaguzi wakitoa ushirikiano wa kutosha.

Katibu wa CCM Kata ya Ndembezi Pendo John Sawa, amesema kuwa wagombea wote walipata fomu na kurejesha zikiwa zimekamilika huku akisisitiza kuwa zoezi hilo limeendeshwa kwa ushirikiano  na usimamizi bora.

“Tarehe 29 mwezi wa kumi wagombea wetu wa nafasi ya wenyeviti tulichukua fomu na wajumbe katika mitaa yote sita leo tumerejesha fomu hizo tukiwa tumezijaza kikamilifu natoa shukrani kwa wasimamizi wa serikali kwa kutupokea vizuri na kutuonyesha ushirikiano wa dhati. amesema Sawa.

“Mama Samia alisema tume ni huru na sisi tunaona kwa vitendo tunasubiri kwa hamu hatua inayofuata ya uteuzi na tuko tayari kuanza kampeni na mikutano ya hadhara kukinadi chama chetu.”amesema Pendo Sawa

Katika hatua nyingine, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Kata hiyo, Issa Said Stima, amewataja wagombea waliorejesha fomu zao kama ishara ya kujiandaa kwa mchakato huo. Wagombea hao ni Onesmo Mahenda Ruhende (Butengwa), Mariam Mikidadi Mdoe (Ndembezi), Bakari Juma (Mabambase), Seif Nassor Hamed (Mbuyuni), Tabitha Costantine Shilingi (Tambukareli), na Solomon Nalinga Najulwa (Dome).

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu ili kuweka viongozi wanaowaamini na wenye nia ya kuleta maendeleo. 



 

Previous Post Next Post