Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa usimamizi na utekelezaji na uratibu mzuri wa uandikishaji wa daftari la wakazi (wapiga kura serikali za mitaa 2024).
DC Mtatiro ameyasema haya leo Oktoba 15,2024 kwenye kikao kazi cha uhamasishaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura serikali za mitaa 2024 kilichowakutanisha Wakuu wa Taasisi,wakuu wa idara na vitengo,Kamati ya ulinzi na usalama, watendaji wa kata,maafisa elimu kata,wakuu wa shule, maafisa elimu msingi na sekondari Pamoja na waganga wafawidhi ndani ya Manispaa ya Shinyanga.
“Tangu zoezi la uandikishaji wapiga kura serikali za mitaa limeanza mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga Mwl. Kagunze amefanya kila kitu, matangazo kila siku yanapita mtaani,redio zinarusha matangazo kila siku,kwa Manispaa ya Shinyanga kama kunawananchi hawatajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura yatakuwa ni maamuzi yake binafsi namshukuru sana Mhe. Rais kumteuwa mkurugenzi huyu msikivu, mchapa kazi,mimi kama Mkuu wa wilaya najivunia kuwa na mkurugenzi kama huyu ndani ya wilaya hii asante sana Mhe. Rais.” amesema DC Mtatiro.
Katika hatua nyingine DC mtatiro amewataka wakuu wa vitengo na taasisi kuhakikisha watumishi wote walio chini yao wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi bora kwa usitawi wa taifa.
Zoezi la uandikishaji wa daftari la wakazi (wapiga kura Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024) limeanza Oktoba 11,2024 ambalo litahitimishwa Oktoba 20,2024.