KAMATI YA SIASA NYANG’HWALE YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA SERIKALI KUU


 Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Nyang’hwale, mkoani Geita, imekagua na kupongeza utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali kuu. Kamati hiyo imeeleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa kusimamia miradi hiyo chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).


Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari ya Kanegele, nyumba mpya ya watumishi aina ya two in one, na ujenzi wa shule mpya, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyang’hwale, Alhaji Adam Mtole, alimsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kikamilifu.



Mtole alibainisha kuwa miradi hiyo inalenga kuimarisha huduma muhimu kwa wananchi na kutatua changamoto zilizokuwepo, hususan katika sekta ya elimu na makazi ya watumishi.




Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani humo, Said Madoshi, alisisitiza umuhimu wa usimamizi thabiti wa miradi ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita. Alitoa wito kwa watendaji kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa wananchi.



Previous Post Next Post