Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU TAWALA WILAYA YA SHINYANGA AWAHIMIZA JESHI LA SUNGUSUNGU KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI

Makamanda wa Jeshi la jadi la Sungusungu wamehimizwa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili wapate sifa za kuwachagua viongozi wao wa vijiji na vitongoji kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika  Novemba 27, 2024.

Jeshi hilo limehimizwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bw. Said Kitinga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo wakati wa mkutano wake na jeshi hilo kiwilaya   uliofanyika katika Shule ya Msingi Lyabukande, Kata ya Lyabukande, Tarafa ya Nindo leo Oktoba  19, 2024.

Zoezi la uandikishaji lilianza tarehe 11 Oktoba, 2024 na litahitimishwa leo Oktoba 20, 2024 .









Post a Comment

0 Comments